“Mapato ya ndani ya halimashauri zetu nayo yameongezeka bilioni 402.66 mwaka 2015/16, hadi shilingi bilioni 661 mwaka wa fedha wa 2019,hii imefanya mapato ya ndani kiujumla yaongezeke kutoka trilioni 11 mwaka 2014/15, hadi shilingi trilioni 18.5 mwaka wa fedha 2018/19"@MagufuliJP
"Najua kulikuwa na hofu lakini Bunge hili liliendelea, najua kuna wengine walikimbia, na sijui kama wamerejea, maana kukimbia sio sahihi, kukimbia changamoto ni ishara ya udhaifu, ni uoga na pia kukimbia ni kutokujiamini.” Rais Magufuli
"Nina imani kubwa Watanzania wataendelea kutuamini na kutupa dhamana ya kuendelea kuongeza nchi yetu ktk vipindi vingine vijavyo na ninaamini katika misingi ya ukuaji wa uchumi tuliyoieweka, nchi yetu katika miaka 5 ijayo tutafanya makubwa zaidi" - @MagufuliJP
#JPMKuvunjaBunge
"Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kutoka tani 15,528,820 kwa mwaka 2015 hadi 16,891,974 mwaka 2018/19. Mahitaji ya chakula kwa mwaka ni chini ya tani milioni 14. Uzalishaji mazao ya Biashara umeongezeka kutoka tani 796,502 hadi tani 1,144,163.1" Rais @MagufuliJP
"Tumeongeza uzalishaji wa miche ya mazao ya kimkakati. Tumejenga na kukarabati skimu za umwagiliaji na vihenge vya kuhifadhi mazao. Tumefufua masoko ya mazao, tumetafuta masoko na tumeimarisha vyama vya ushirika." - Rais @MagufuliJP
"Sanaa na Burudani ziliongoza kwa ukuaji. Mwaka 2018 ilikuwa kwa 13.7%, 2019 ilishika nafasi ya 3 kwa ukuaji wa 11.2%. Hongereni sana wasanii wetu hususani Bongofleva, filamu, mpira nk, kazi zenu sio tu zinaburudisha na kuchangia uchuki ila zinaitangaza Nchi." Rais @MagufuliJP
"Mapato yatokanayo na madini yameongezeka mwaka 2018/19 zilikusanywa Bil 346, kutoka Bil 194, mwaka huu wa fedha 2019/20 tunatarajia kukusanya Bil 470 ambapo April pekee licha uwepo wa tatizo la Corona tumekusanya Bil 58 haijawahi kutokea" - Rais @MagufuliJP
#JPMKuvunjaBunge
"Idadi ya watalii na mapato yameongezeka, 2019 tulipokea watalii zaidi ya Mil 1, mapato yameongezeka kutoka Dola Bil 1.9 2015 hadi Dola Bil 2.6 mwaka 2019, isingekuwa Corona mwaka huu pia idadi ya watalii na mapato yake yangeongezeka maradufu" - Rais @MagufuliJP
#JPMKuvunjaBunge
“Naipongeza Timu yetu ya Taifa ya Soka ambayo baada ya takribani miaka 39 kupita hatimaye mwaka jana ilifanikiwa kufuzu kushiriki fainali za kombe la Afrika,nawapongeza wanamichezo mingine waliopeperusha vizuri bendera yetu hususani katika ndondi na riadha”- Rais Dk. @MagufuliJP
"Tumeimarisha huduma za mawasiliano hususan katika kuboresha usikivu wa simu kutoka 79% mwaka 2015 hadi kufikia 94% mwaka 2019, idadi ya watumiaji wa simu za mkononi pamoja na watumiaji data imeongezeka maradufu "- Rais @MagufuliJP
" Idadi ya Wanafunzi wanaojiunga vyuoni imeongezeka kutoka 65,064 mwaka 2015 hadi 87,813 mwaka 2020. Wanaopata mikopo wameongezeka toka 98,300 2014/15 hadi 130,883 mwaka 2019/20. Nitakuwa sijakosea nikisema kazi kubwa imefanyika kwenye sekta ya elimu"Rais @MagufuliJP
"Sangara kwenye Ziwa Victoria wameongezeka kutoka Tani 417,936 hadi Tani 816, 964, urefu wake umeongezeka kutoka wastani wa CM 16 hadi CM 25.2 na hivyo samaki wetu kuanza kuhitajika katika soko la Ulaya na ndege zimeanza kuja Mwanza na kubeba" - Rais @MagufuliJP
#JPMKuvunjaBunge
"Tumekamilisha ujenzi wa barabara za kiwango cha lami za kiasi cha kilometa 3,500. Tumeanza kujenga flyovers na interchange kwa kuanzia Dar es Salaam ili kupunguza msongamano." - Raia @MagufuliJP
#kuvunjwaKwaBungeLa11
"Tumeboresha usafiri wa maji kwenye maziwa yetu makuu. Tumekarabati meli 5 katika Ziwa Victoria; tunaendelea kujenga meli ya MV Mwanza. Tumekarabati meli ya Mafuta katika Ziwa Tanganyika na MV Liemba inaendelea kukarabatiwa." - Rais @MagufuliJP
#KuvunjwaKwaBungeLa11
"Tumefufua ATCL kwa kununua ndege mpya 11 na ambapo 8 zimefika na nyingine zinatengenezwa. Faida nyingine ya ndege tumeiona katika kipindi hiki cha Corona ambapo Watanzania mbalimbali waliokwama ikiwemo India tumewarejesha." - Rais @MagufuliJP
#KuvunjwaKwaBungeLa11
"Tumeboresha upatikanaji wa nishati ya umeme. Ujenzi wa mradi wa Julius Nyerere Hydropower Station unaendelea ingawa ulipigiwa kelele sana. Pesa zote za ujenzi ni za Watanzania. Umetumia Tsh. 6.5 trilion na unaweza kuzalisha 2,115 MegaWatts." - Rais @MagufuliJP
#KuvunjwaKwaBunge
"Nakumbuka kuna wakati Waziri Mpina alikuwa anatembea na rula kwenye migahawa, lakini ilikuwa ni katika kazi ya kuhakikisha tunapata mafanikio, zaidi ya hapo tumefanikiwa kuongeza idadi ya wafugaji wa samaki kutoka 18,843 hadi 26,474, 2020" - Rais @MagufuliJP
#JPMKuvunjaBunge
"Katika kipindi cha miaka 5 iliyopita tumejitahidi kukuza sekta kuu za uchiumi na uzalishaji ikiwemo viwanda, kilimo, biashara, madini na utalii, tumejenga viwanda vipya 8,477, vikubwa 201, vya kati 460, vidogo 3,406 na vidogo sana ni 8,410" - Rais @MagufuliJP
#JPMKuvunjaBunge
0 Comments