Na Amiri kilagalila,Njombe
Akitolea ufafanuzi wa namna wananchi walivyokuwa
wakikabiliwa na adha mbalimbali ndani ya jimbo la Lupembe, aliyekuwa mbunge wa
jimbo hilo kabla ya kuvunjwa kwa bunge hilo leo Mh,Joram Hongoli ameishukuru
serikali ya awamu ya tano kwa kupeleka fedha nyingi katika miradi ya afya,
elimu, maji pamoja na barabara ndani ya wilaya ya Njombe pamoja na kukamilisha
ujenzi wa hospitali ya wilaya iliyojengwa Matebwe wilayani humo.
Ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Njombe imetajwa
kuwa mkombozi wa upatikanaji wa huduma za afya pindi itakapoanza kutoa huduma.
“Sio muda wiki lililopita tayari tumeshapata milioni
300 kwa ajili ya ukamilishaji ili hospitali ile ianze kufanya kazi”alisema
Hongoli
Wakazi wa Matembwe akiwemo Petronia Mtega na Rozena Gidion
wamezungumza hatua ya serikali kujenga hospitali hiyo katika eneo lao kwa
gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 na kwamba itasaidia sana kupungunguza
changamoto ya usafiri wa kwenda mbali kufuata huduma za afya.
“Kwa hiyo sisi tunaona wametupunguzia ile ghalama ya
kupanda magari mpaka Kibena kwa hiyo ikiinza tutaanza kupata huduma hapa jirani
tunashukuru pia mbunge wetu kwa kutupigania”alisema Petronia Mtega
Kwa upande wa upatikanaji wa maji safi na salama
kwenye vijiji na kata, wananchi hao akiwemo Riziki Msoso na Furaha Nduye
wamesema licha ya kazi kubwa kufanyika katika serikali hii ya awamu ya tano
lakini inapaswa kuongezwa nguvu katika utekelezaji wake.
“Lakini mpaka sasa tunaamini kwa jitihada za
mheshimiwa Rais tunashukuru sana kwasababu awali maji ilikuwa ni tatizo kubwa
sana lakini sasa asilimia nyingi seheu nyingi zinapata maji”alisema Riziki Msoso
0 Comments