TANGAZA NASI

header ads

CHADEMA wadai kuto jibiwa ombi la ulinzi kwa ajili ya lisu ili arejee nchini




Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  kimedai kuto jibiwa Ombi lao la ulizi kwa ajili ya makamu mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lisu kwa ajili ya kurejea nchini.

Hayo yamebainishwa na Katibu mkuu wa Chadema John Mnyika wakati akizungumza na waandishi wa habari hii leo

"Disemba 23, 2019, nilimuandikia barua rasmi IGP kuomba ulinzi wa Polisi kwa ajili ya Makamu Mwenyekiti bara wa chama ambaye amekuwa akiishi nje kwa matibabu aweze kurudi, lakini mpaka leo hatujapatiwa majibu ya ombi letu" -
Katibu Mkuu wa

Mnyika ameendelea kusema kuwa

"Kama kuna ushahidi wa wanayoyasema kuhusu tukio la kushambuliwa kwa
basi watoe ushahidi na mashahidi. Kuna maneno maneno haya ya kusema alikuwa amelewa basi madaktari waliompokea waseme" -
Katibu Mkuu wa

"Katika wakati muafaka sisi kama chama tutawaongoza wananchi kuhusu uchaguzi huu ujao na tutazilinda kura zetu kuhakikisha kwamba haki inatendeka na mabadiliko yanatokea" -
Katibu Mkuu wa
"Katika tukio la kushambuliwa Mwenyekiti

kwa mara nyingine tena Jeshi la Polisi limejaribu kuonesha kama vile hakushambuliwa na kwenda mbali zaidi kusema wanakusudia kumpeleka mahakamani" -
Katibu Mkuu wa


Post a Comment

0 Comments