Na Furahisha Nundu,Makete
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kusini Kati imedhamiria kugawa vifaa Kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona,vifaa vyenye thamani zaidi ya shilingi Milioni 150 Wilayani Makete mkoani Njombe
Vifaa hivyo ni pamoja na Ndoo za maji,Vitakasa mikono (Sanitizer), Barakoa sambamba na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya homa kali ya mapafu kwa viongozi wa Dini kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kusini Kati na watendaji wa vijiji.
Askofu wa KKKT-DKK Mch.Wilson Sanga amesema mpango huo wa utoaji elimu unatarajia kuwanufaisha wananchi wasiopungua 400 katika baadhi ya Majimbo ya Dayosisi hiyo pamoja na watu wenye mahitaji maalum kama wazee na walemavu.
Imeelezwa kuwa baadhi ya wananchi Kata ya Ipepo na Mbalatse Wilayani Makete wamekuwa wakipuuzia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa Afya ktk mapambano dhidi ya Homa kali ya mapafu
Kwa mujibu wa viongozi na wawakilishi wa wananchi vijiji vya Kata hizo Jimbo la Mashariki Lupila wamesema Hali ya upuuziaji wa maelekezo ya wataalamu iko juu na kufanya watu kutochukua tahadhari katika kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona.
Elay Sanga mchungaji wa usharika wa Ilungu na Laurent Bangulinyi mwenyekiti wa kijiji Maliwa wamesema wananchi wengi vijijini hawajui umuhimu wa kutumia vifaa Kinga kama uvaaji wa Barakoa,kunawa mikono na matumizi ya vitakasa mikono Sanitizer pamaja na kwamba wamekuwa wakipewa maelekezo ya kitaalam mara kwa mara
Hayo yamebainishwa na wataalam wa Afya wakiwa na viongozi wa Dini walipofika Jimbo la Mashariki Lupila kutoka elimu jinsi ya kujikinga na Maambukizi ya Homa kali ya mapafu katika sharika za Jimbo Hilo.
Sergio Nkwama mtaalamu wa masuala ya Afya kutoka Hospitali ya Wilaya ya Makete ameweka msisitizo wa kufuata utaratibu wa kunawa,kuvaa Barakoa na kuendelea kusisitiza uchukuaji wa hatua za kupambana na Maambukizi ya COVID 19
Majimbo sita tayari yameanza kunufaika na msaada huo,ambayo ni Jimbo la Kaskazini Makete, Jimbo la kusini Utengule, Jimbo la Kati Bulongwa, Jimbo la Magharibi Iniho/Ipelele, Jimbo la Mashariki Lupila na Jimbo la Mashariki kati Tandala
0 Comments