SALVATORY NTANDU
Imebainishwa
kuwa Mikopo yenye riba ya juu na isiyokuwa na mikataba inayotozwa na
Taasisi za Kifedha mkoani Shinyanga inachangia kukwamisha utendaji kazi
wa Walimu katika Vituo vyao vya kazi kutokana na baadhia yao kudaiwa na
taasisi hizo.
Hayo
yamebainishwa Mei 14 mwaka huu na katibu wa Chama cha Walimu Manispaa
ya Shinyanga, James Peter katika Mkutano (CWT) uliofanyiaka Mjini humo
na kufafanua kuwa ofisi yake inamashauri mengi yenye malalamiko ya
walimu kudaiwa fedha na Vikundi vya ukopeshaji fedha (SACCOS) pamoja na
baadhi ya Mabenki .
Alisema
kuwa wengi wao wanatozwa riba za juu ambazo zinasababisha washindwe
kufundisha kwa ufanisi katika vituo vyao vya kazi hali ambayo imekuwa
ikisababisha migogoro isiyokuwa na tija na waajiri wao pindi
wanapofanyiwa ukaguzi.
“Tumebaini
Kuna walimu wamekopeshwa fedha na Taasisi hizi bila ya kuwa na mikataba
ya ukopeshaji hali ambayo inasababisha waendelee kukatwa fedha kwa
muda mrefu hata kama wamemaliza kulipa madeni yao,huku wengine
wakidiriki kushikilia kadi zao za benki,”alisema James
James
alifafanua kuwa ni wakati sasa wa Walimu mkoani humo kuitumia benki ya
walimu ili kujipatia mikopo kwa riba nafuu ambayo itawasaidia kujikwamua
kimaisha hususani katika kipindi hiki cha uwepo wa janga la ugonjwa wa
homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona.
Awali
akifungua mkutano huo, Katibu wa Cwt Mkoa wa Shinyanga,Mwalimu Lazaro
Tuliasaulo aliwataka walimu kuachana na mikopo isiyokuwa na tija
sambamba na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya maendeleo ambayo
inaweza kuwapatia fedha za kujikimu.
“Tumieni
kipindi hiki ambacho shule zimefungwa kutokana na COVID 19 kuaibua
miradi ya ujasiriamali itakayowawezesha kupata fedha achaneni na mikopo
ambayo inasababisha mfukuzwe kazi na waajiri wenu tumieni maarifa
mliyonayo katika vituo vyenu vya kazi kujipatia fedha kwa njia zilizo
halali,”alisema Tuliasaulo.
Nae
Raymond Shimiyu Mwalimu kutoka shule ya sekondari Mwisela amewaomba
walimu kutumia asilimia 15 ya fedha zinazotolewewa na CWT kwa matawi
katika vituo vyao vya kazi kwa kuanzisha miradi ya maendeleo na kuachana
na tabia ya kuzigawana fedha hizo ambazo zinaweza kuwasaidia.
“Fedha
hizi zinatosha kuanzisha miradi ya ufugaji,kilimo na viwanda vidogo
naomba CWT itoe mwongozo ili zitumike kama ilivyokusudiwa maana kwa sasa
huwa tunazigawana katika shule zetu pindi zinapotolewa,”alisema
Shimiyu.
Zaidi
ya walimu 50 wanadaiwa fedha mbalimbali na taasisi hizo ambapo
wanasheria wa CWT wanaendelea kuyahakiki madeni hayo ili kujiridhisha na
uhalali wake kutokana na baadhi yao kubainika kuendelea kukatwa fedha
licha ya kumaliza madeni yao.
0 Comments