TANGAZA NASI

header ads

Makambako:Wazee walalamika kuathirika kiuchumi zaidi kutokana na Corona

Is COVID-19 eroding China's Influence in Southeast Asia? - Belt ...

Na:Clief Mlelwa,Makambako

Baadhi ya wazee katika halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe wamekiri kuathirika kiuchumi kutokana na uwepo wa janga la Corona ambalo limesababisha muda mwingi wakae nyumbani ili kujikinga na ugonjwa huo.

Baadhi ya wazee hao wanaoishi katika mtaa wa Kikula,Sigridi na Magegele mjini Makambako,wamesema kuwa kutokana na wao kutajwa kuwa ni kundi moja wapo linaloweza kupata maambukizi ya virusi hivyo kwa haraka imewalazimu wabakie majumbani hali ambayo imeathili kipato chao cha kila siku.

Aidha wazee hao wamesema kuwa kutokana na tahadhari hiyo ya kubakia nyumbani muda wote imepelekea washindwe hata kupata fedha kwa ajili ya kununulia vifaa tiba vya kujikinga na virusi vya Corona hasa barakoa.

Nao wananchi wa halmashauri ya mji wa Makambako wamesema kuwa jamii kwa ujumla ina kila sababu ya kuungana pamoja ili kuwasaidia wazee hao kwa kupatiwa vifaa tiba hata chakula.

Naye afisa mtendaji wa kata ya Makambako ALFRED MWALONGO amewataka vijana kuwakumbuka wazazi wao hasa katika kipindi hiki cha kukabiliana na Corona kwa kuhakikisha wanakuwa na mahitaji yote ya msingi.

Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Makambako ALEXNDER MCHONE amesema kuwa wazee wapo kwenye hatari ya kupata virusi hivyo vya Corona kama hawatachukua tahadhari kwa kuwa kinga zao za mwili ni ndogo.


Post a Comment

0 Comments