Na.WAMJW- Dar es Salaam
Wamiliki
wa viwanda vya Dawa, Vifaa na vifaa tiba nchini wametakiwa kuanza
kuzalisha vifaa kinga kuweza kukabiliana na janga la Corona nchini ili
kuondokana na changamoto ya ucheleweshaji wa kupata vifaa kinga toka nje
ya nchi pamoja na kupunguza gharama.
Wito
huo umetolewa leo jijini hapa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiongea na Umoja wa
Wazalishaji Dawa, Vifaa na Vifaa Tiba (TPMA) nchini kwenye mkutano wa
kuangalia jinsi gani wanaweza kuzalisha vifaa kinga kutoka wazalishaji
wa ndani hapa nchini.
“Tukizalisha
hapa nchini tutaokoa rasiliamali fedha nyingi, muda pia tutazalisha
ajira na kuwa na uhakika wa ubora na usalama unaohitajika kupitia
mamlaka zetu za ndani kwa urahisi”. Alisema Waziri Ummy.
Waziri
amesema kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa kinga , hivyo wale wote
wanaozalisha vifaa kinga wanatakiwa kuongeza uzalishaji ili kutosheleza
mahitaji ya soko nchini na hata kuweza kuuza nchi za jirani.
Aidha,
amesema Wizara inahitaji kuipa nguvu huduma salama kwenye vituo vya
kutolea huduma za afya vya serikali na visivyo vya Serikali kwa
watumishi wa afya kuzingatia miongozo ya kukinga na kudhibiti maambukizi
angalau kuvaa barakoa,glove na eproni hivyo amewasisitiza kuzalishaji
vifaa vyenye viwango vyenye ubora ili kukidhi soko la ndani nan chi za
jirani.
Naye
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa amewapongeza wamiliki
wa viwanda hivyo kwa kubuni na kugundua teknolojia na uzalishaji wa
vifaa kinga kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo.
“Kuanzisha
viwanda ni sehemu ya ulinzi wa nchi,hivyo kuwa na viwanda vyetu nchini
hususani wakati wa shida imesaidia upatikanaji wa baadhi za vifaa kinga
kwa bei nafuu”.Alisema Waziri Bashungwa
Amesema
katika kikao hicho wamekubalia kujipanga vizuri katika uzalishaji wa
vifaa kinga na hivyo wamewataka Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC)
kujikita katika kuzalisha barakoa aina ya N95 na glove kutokana na
kwamba viwanda vya namna hii havipo nchini.
Pia
Waziri Bashungwa ameitaka TMDA kushirikia na wizara ya viwanda
kuisaidia NDC kuweza kufanya kiwanda hicho kuanza kuzalisha kwa wakati
na hivyo kusaidia watumishi wa afya walio mstari wa mbele kutoa huduma
bila hofu.
Kwa
upande wa MSD, Waziri Bashungwa ameitaka kununua vifaa kinga
vinavyozalishwa na viwanda vya ndani ambavyo vimekidhi viwango na
vimesajiliwa na TMDA badala ya kutumia fedha iliyotengwa na Serikali
kununua vifaa hivyo nje ya nchi.
Waziri
Bashungwa ameahidi kukitembelea kiwanda cha Msagala Investment
kilichopo Bagamoyo ambacho kinatarajia kuanza kuzalisha malighafi za
utengenezaji wa barakoa kutokana na pamba zinazolimwa nchini.
0 Comments