
SIMBA
wapo tayari kwa utaratibu wowote utakaotolewa na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) ikiwemo suala la upimaji wa afya ili kujiridhisha kuwa
wachezaji wao wote akiwemo Meddie Kagere na Aishi Manula hawana
maambukizi ya Virusi vya Corona kabla ya kuendelea kwa michuano ya Ligi
Kuu Bara.
Kauli
hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa ikiwa ni siku
chache baada ya Serikali kuruhusu michezo kuendelea Juni Mosi, mwaka
huu.
Senzo
amesema: “Tunaheshimu maamuzi yaliyotolewa na Serikali, tumejiandaa na
tuko tayari kwa ajili ya kuendeleza kampeni yetu ya kusaka ubingwa wa
Ligi Kuu Bara.
"Kwa
sasa tunasubiri TFF na Bodi ya Ligi watupe utaratibu wa namna gani
tutarejea uwanjani na tutatoa ushirikiano wa kutosha hata ikihitajika
kupima afya za wachezaji wetu."
Hivi
karibuni, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison
Mwakyembe, alisema wamepanga baada ya ligi kurudi, vitumike viwanja vya
Taifa, Uhuru na Azam Complex jijini Dar kwa mechi za Ligi Kuu Bara
pekee, huku Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zitumie CCM
Kirumba na Nyamagana jijini Mwanza.
0 Comments