TANGAZA NASI

header ads

Kijana Mbaroni kwa tuhuma za kupasua kichwa na kumwagika kwa ubongo wa babu yake



Na Amiri Kilagalila,Njombe

Jeshi la polisi mkoani Njombe,linamshikilia kijana Imani Mbilinyi (25) mkazi wa kijiji cha  Maleutsi mji mdogo wa Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe  kwa tuhuma za mauaji akituhumiwa kumpasua kichwa babu yake aitwaye Elia Mbilinyi (90) na kisha kuutoa ubongo wake karibu na nyumbani kwao.

Tukio hilo la kikatili limetokea usiku wa kuamkia  Oktoba 14, 2020 majira ya saa mbili usiku ambapo inatajwa kuwa mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauji hayo akamua kujisalimisha kwa mwenyekiti wa mtaa wa Luswaganga katika kijiji hicho kama anavyoeleza mtendaji wa kijiji cha Maleutsi bwana Michael Mnzengwasanga 

"Jana tulipewa taarifa kwamba kijana huyo amefanya maujai ikabidi tumkamate na kutoa ripoti kituo cha polisi na walichukua jitihada za kututafuta na kumchukua mtuhumiwa,kwakweli tuligundua mzee amelala amechokonolewa ubongo na uzuri wake kijana alipofanya mauaji alikuja kujieleza yeye mwenyewe kirabuni"alisema Michael Mnzengwasanga afisa mtendaji kijiji cha Maleutsi

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Usadanga bwana Exavery Mbilinyi yalikotokea mauaji hayo, amesema baada ya kuelezwa taarifa hizo  akaamua kuwaita mgambo wa kijiji wkamuweka chini ya ulinzi na kisha wakatoa taarifa polisi ambao walifika usiku huo kuja kumchukua mtuhumiwa huyo

"Nilikuwa nimekaa kirabuni akaja huyu kijana aliyefanya mauaji akaniuliza mwenyekiti ninaweza kutamka jambo ukanilinda,akasema tuongee nje,kutoka nje nikaona ana damu,akasema mimi kule nyumbani nimeua nikamwambia umeua nini hakusema akaingia ndani,nikawa na wasi wasi nikaita mgambo wakamfunga kamba na kuongoza mpaka nyumbani alikofanya mauaji ambayo ni ya babu yake"alisema Exavery Mbilinyi 

Mmoja wa wanafamilia wa marehemu bwana Fulamu Mbilinyi pamoja na balozi wa mtaa huo wamezungumzia namna walivyopokea taarifa za kifo cha Mzee wao huku wakibainisha kuwa hakukua na mgogoro wa aina yoyote baina ya mtuhumiwa na marehemu ambaye ni babu yake.

"Ni masikitiko tu kwa kuwa mzee hakuwa na ugomvi na mtu basi tu tunashangaa kwasababu mtu mwenyewe aliyemuua ni mjukuu wake wa mtoto wake wa kwanza alikuwa anaisha Sumbawanga huku alirudi kimatatizo alikuwa amechanganyikiwa toka alikotoka na ni mvutaji wa sigara"alisema Fulamu Mbilinyi 

Kwa upande wake Daktari Nolasisi Haule kutoka hospitali ya wilaya ya Makete ambaye ndiye aliyeufanyia uchunguzi wa mwili wa marehemu amezungumzia sababu zilizopelekea kifo  cha mzee huyo.

"Nimeangalia maiti,miguu iko vizuri na tumbo liko vizuri kasoro ubongo umetolewa kwenye ubongo umetapakaa nje ya  mwili,yaani amevuja damu nyingi na mjukuu wake hayupo sawa ni mvuta bangi,anavuta sigara na anakunywa sana pombe"alisema Daktari Nolasisi 

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akieleza kuwa hatua za kisheria zitachuliwa dhidi ya mtuhumiwa sambamba na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

"Kweli tukio hili limetokea na inaonyesha huyu mjukuu hana baba wala mama na ana tabia ya kupoteza kumbu kumbu,alimvizia babu yake akampiga mti wa kichwa na kichwa kikapasuka,na imeingia imani ya kishirikina huyo kijana yuko mbaloni na hatua za kisheria zinachuku dhidi ya tukio hilo"alisema Kmanda Issa

Post a Comment

0 Comments