Na Amiri Kilagalila,Njombe
Ikiwa leo Oktoba 15, 2020 ni kumbu kumbu ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, Deo Filikunjombe aliyefariki kwa ajali ya Ndege mwaka 2015 wakati akitekeleza majukumu yake ya kampeni za uchaguzi.Mgombe ubunge wa jimbo hilo aliyepita bila kupingwa wakili Joseph Kamonga amuombea rehema.
Aidha Kamonga ametoa wito kwa wananchi wa jimbo hilo kuendelea kumuombea huku akishukuru watangulizi wake kwa kazi kubwa walizofanya ndani ya jimbo hilo.
Kamonga ametoa wito huo akiwa kwenye mkutano wa kampeni za kumuombea kura Rais Dkt,John Pombe Magufuli na madiwani wa CCM katika kata ya Mkongobaki.
"Tuzidi kumwombea yeye na wabunge wote wa Ludewa kwasababu kila mmoja ana mchango kwa maendeleo ya Ludewa mpaka tukafika hapa,natambua namna ambavyo marehemu Deo Filikunjombe alivyokaa kwa wanaludewa ndani ya mioyo yao basi bado wanamkumbuka zaidi"alisema Kamonga.
Aidha mapema asubuhi ya leo wakili Joseph Kamonga alihudhuria misa takatifu ya kumuombea mbunge huyo wa zamani ambaye sasa anatimiza miaka mitano tangu kifo chake.
Vile vile akizungumza katika misa hiyo iliyofanyika katika kanisa Katoriki Mkongobaki,amempongeza marehemu Filikunjombe kwa kazi nzuri aliyoifanya enzi za uhai wake na amewataka wananchi kuanzia kesho hadi Jumapili kuwaombea wabunge wengine waliotangulia mbele za haki ili kuuenzi mchango wao wa maendeleo.
0 Comments