Ufaransa imetangaza kuwa siku ya Jumamosi itaanza kutekeleza marufuku ya kutotoka nje usiku kwenye mji mkuu Paris na miji mingine 8 mikubwa katika juhudi zake za kukabiliana na janga la virusi vya corona.
Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni, Rais Emannuel Macron wa Ufaransa amesema marufuku hiyo itakuwa kati ya saa tatu usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi na itudumu kwa hadi muda wa wiki sita.
Macron amesema lengo la hatua hiyo ni kupunguza maambukizi ya COVID-19 kutoka wastani wa sasa wa visa 20,000 kwa siku hadi angalau visa 3,000 au 4,000 idadi ambayo inaweza kudhibitiwa.
Kiongozi huyo amesema ingawa Ufaransa haijashindwa kudhibiti janga la COVID-19 ambalo tayari limewauwa watu 29,000 nchini humo, lakini anatiwa wasiwasi na wimbi la maambukizi linaloendelea kuitikisa nchi hiyo.
0 Comments