Marcus Rashford alitunukiwa tuzo kwa kampeni yake ya kupata chakula cha bure kwa ajili ya watoto wakati wa likizo nchini UingerezaImage caption: Marcus Rashford alitunukiwa tuzo kwa kampeni yake ya kupata chakula cha bure kwa ajili ya watoto wakati wa likizo nchini Uingereza
Chakula bure cha shule kitakuwa kikitolewa kwa watoto wakati wa likizo katika eneo la wales hadi mwezi Aprili 2021, imetangazwa .
Mchezaji soka wa England Marcus Rashford, ambaye alifanikiwa katika kampeni ya suala la ugawaji wa chakula kwa wanafunzi nchini Uingereza, amepongeza mpango huo.
Waziri wa elimu wa Uingereza Minister Kirsty Williams amesema pauni milioni 11 zitalipia mpango wa utoaji wa chakulakwa wanafunzi ikiwa ni pamoja hadi wakati wa likizo ya Pasaka mwaka 2021.
Nyota huyo wa Manchester United amesema mpango huo utasaidia "watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini".
Zaidi ya wanafunzi 75,000 wenye umri kati ya miaka mitano na 15 kutoka familia zenye kipato cha chini wanastahili kupata chakula cha bure kote Wales.
Mpango huo pia uko wazi kwa watoto wadogo zaidi wanaohudhuria masomo ya chekechea kwa siku nzima.
0 Comments