TANGAZA NASI

header ads

Serikali mpya ya Israeli kuapishwa leo

 
Hatimaye serikali mpya ya Israel itaapishwa hii leo baada ya taifa hilo kurudia uchaguzi mara tatu. Benjamin Netanyahu, waziri mkuu aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi nchini humo, anaendelea kusalia kwenye nafasi yake akishirikiana na mpinzani wake Benny Gantz.
  Wawili hao watakuwa wakiongoza kama mawaziri wakuu kwa awamu. Netanyahu wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud anayekabiliwa na kesi ya rushwa itakayoanza kusikilizwa wiki ijayo, atakuwa wa kwanza kuiongoza serikali mpya kwa kipindi cha miezi 18.

Kisha mpinzani wake Gantz, wa chama cha muungano wa siasa za wastani wa Bluu na Nyeupe anatarajiwa kupokea nafasi hiyo ifikapo mwezi Novemba mwaka 2021.

Post a Comment

0 Comments