TANGAZA NASI

header ads

SERIKALI KUONGEZA UWEKEZAJI KWA KUONDOA KERO YA KODI NA TOZO ZA MIFUGO NCHINI


Serikali imepanga kufanya marekebisho katika kodi,tozo na ada mbalimbali ambazo zimekuwa kero kwa wazalishaji na wafanyabiashara wa mifugo na mazao ili kuhamasisha uwekezaji katika sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina wakati akiwasilisha makadirio, mapato na matumizi ya wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa Fedha 2020/2021 na kuliomba bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 66.82.

Mhe.Mpina amesema kuwa marekebisho hayo yatafanyika baada ya watalaamu wake katika sekta hiyo kufanya tathimini na kuanza kutumika rasmi ili wawekezaji, wazalishaji na wafanyabiashara wa mifugo na mazao kunufaika na serikali yao kwani ipo kwa ajiri ya kuwatumikia watanzania.

 Mhe. Mpina amesema kuwa kutokana na malalamiko ya wadau juu ya viwango vikubwa vya kodi, ada,ushuru na tozo wizara imeamua kufanya mapitio ya kanuni zake ili kuondoa changamoto hizo kwa wadau wake.

Mhe Mpina amesema kuwa mwaka wa fedha 2020/2021 Wizara inatarajia kufanya maboresho ya ada mbalimbali za leseni za wavuvi kwa lengo la kuwapa unafuu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika sekta ya uvuvi.

“Uboreshaji wa ada za leseni na tozo za uvuvi unalenga kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya uvuvi na kukuza biashara ya samaki, mazao yake na kuinua uchumi wa taifa” ameeleza Mhe. Mpina.

Aiha Mhe. Mpina amesema kuwa idadi ya watumishi wa ugani katika sekta ya mifugo bado ni ndogo ikilinganishwa na mahitaji.

“Mahitaji ya wataalamu wa ugani wa mifugo kwa sasa ni 17,848 lakini idadi hii ya wagani wa mifugo waliyopo kwa sasa katika mikoa na mamlaka za serikali za mitaa ni 3,795 hivyo kuwa na upungufu wa wagani 14,053”, amebainisha Mhe. Mpina.

Katika hitimisho lake Mhe. Mpina amesema katika mwaka wa fedha 2010/2020 juhudi za kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli kutokana nauvuvi wa bahari kuu zilifanyika ikiwa ni Pamoja na serikali kuondoa tozo ya dola za kimarekani 0.4 kwa kilo ya samaki.

Post a Comment

0 Comments