Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Salum Hamduni, amesema kuwa
mara baada ya Mwalimu Agnes Mushi, anayetuhumiwa kumpiga mwanamke
mwenzake kwa madai ya kwamba amemfumania na mumewe, kukiuka wito wa
jeshi hilo, basi Polisi wataingia wenyewe kumsaka popote alipo na
kumkamata.
Kamanda Hamduni ameyabainisha hayo leo Mei 27, 2020na kuongeza kuwa mara
baada ya kukamilisha upelelezi wale wote waliokuwepo eneo la tukio,
ikiwemo wale walioshiriki kurekodi video na kuisambaza kwenye mitandao
ya kijamii watafikishwa kwenye mkono wa sheria.
"Huyu mama hajaripoti, tunaendelea na ufuatiliaji wa mbinu nyingine ili
kuweza kumfikisha kwenye vyombo vya sheria, sisi tunashughulika na
jinai, na hatutarajii mtu kama anaweza kujipeleka Polisi, ni wajibu wa
Jeshi la Polisi kumkamata, lakini kwa mwananchi aliyestaarabika ni vema
anapopata taarifa za kutafutwa afike, inamuongezea credit hata uwezekano
wa kupata dhamana na haki nyingine na tungemuona kama ni mtu ambaye
anapenda kutii sheria" amesema Kamanda Hamduni.
Aidha akizungumzia kuhusu hali ya mwanamke aliyeshambuliwa kwa tuhuma
hizo za kutembea na mume wa mtu, ACP Hamduni amesema kuwa alifanikiwa
kupata PF3 na alienda kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mawenzi.
0 Comments