TANGAZA NASI

header ads

Njombe:Wakulima waanza kupeleka nguvu kwenye kilimo cha Kitaru Nyumba



Na Joctan Myefu,Njombe

Jamii za wakulima mkoani Njombe zimeanza kuachana na kilimo cha asili na kuamua kujikita katika kilimo cha kisasa kinachotumia teknolojia mpya ya kitaru Nyumba ili kuongeza ubora na kiwango cha uzalishaji wa mazao yenye tija katika soko la ndani na nje ya Nchi.

Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa mitano Tanzania inayozalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara lakini wakulima wengi wamekuwa wakizalisha mazao yanayokosa ushindani sokoni kutokana na kufanya kilimo cha mazoea na asilia.

Wakiweka bayana sababu ya kuacha kufanya kilimo cha mazoea na nguvu kuhamishia katika matumizi ya kitaru Nyumba baadhi ya wakulima akiwemo Tasisius Mdendemi na Gelord Haule wanasema kilimo hicho kinatumia eneo dogo kuleta mazao mengi ambayo yanakuwa na ushindani mkubwa sokoni na kudai kwamba wakati umefika kubadili maisha kupitia teknolojia hiyo.

Licha ya teknolojia ya kitaru nyumba kupokelewa vyema na jamii za wakulima mkoani Njombe lakini kilimo hiki kimetajwa kugharimu fedha nyingi katika uendeshaji wake jambo ambalo linawafanya wengi wao kushindwa kumudu na kuitaka serikali kupitia mikopo ya benki ya kilimo na halmashauri kuona namna ya kuwapa mikopo yenye riba nafuu ili waweze kuingia shambani.

Padre Damas Mahali ni moja kati ya walaji wengi wa mazao yanayozalishwa kwa kutumia teknolijia isiyotumia mbolea za chemikali ambaye anasema wakati umefika kuwekeza zaidi katika kilimo hicho.

Post a Comment

0 Comments