Na Amiri kilagalila,Njombe
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Njombe
kimesema hakijashtushwa na taarifa za Madiwani wao watatu wa wilaya ya Makete
kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM kwa kuwa walishakuwa na taarifa za
kuwa wamekuwa wakitishwa kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe rose mayemba
amesema kuwa licha ya madiwani hao kutotoa sababu hizo hadharani lakini kama
chama kilishapata taarifa hizo kwa muda mrefu kwamba wamekuwa wakitishiwa mara
kadhaa na kuwataka kuachana na chama hicho.
“Taarifa za kuhama kwa madiwani wetu 3 wilayani
Makete,kama chama hatujastushwa kwasababu tulishakuwa na taarifa za awali na
tulijaribu kuhojiana nao na wengi wao walisema kabisa namna ambavyo wanatishwa
na kuhatarishiwa maisha yao na wakaona hawawezi kustahimili na wakaamua
kuondoka kwa hiyo haijatustua na tulishaifuatilia” amesema Rose Mayemba
mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe
Hata hivyo bado kumekuwapo kwa taarifa za muda mrefu
kuwa kuna baadhi ya madiwani wao katika majimbo mengine likiwemo la Njombe Mjini
kuwa wanampango wa kuhamia CCM wakati wowote Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema
tayari wameshakaa nao licha ya kukataa.
“Hata hao wengine tunafahamu na tumezungumza nao ila
wengine wanakataa na wengine wanakiri kwamba CCM wanawafuata na kuwatisha
lakini sisi kama chama tunawaonya CCM sio tabia njema kwa ustawi mzuri wa
demokrasia,wananchi walitakiwa kuacha huru kila mmoja asimame mahali ambapo
kwake ni sahihi japo kuwa pia ni haki ya kikatiba mtu kutoka”alisema tena Rose
Mayemba
Agrey mtambo ni katibu wa madiwani mkoa wa Njombe na
diwani wa kata ya Njombe Mjini ambaye anasema licha ya kuwa madiwani hao
wamehama Chadema kwa mujibu wa katiba lakini wanashangazwa na kitendo hicho
kufanyika ikiwa imebaki mwezi mmoja kumaliza muda wao jambo linalowakosesha
stahiki zao za udiwani.
“Tumebakiwa na mwezi mmoja tu kustaafu lakini Yule aliyetumika
mpaka mwezi wa jana na kuhamia chama kingine tafsiri yake sio mwanachama wa
Chadema,taratibu za kimaslahi binafsi zitakuwaje hatujui”alisema Mtambo
hata hivyo diwani mtambo amekanusha taarifa za kuwa
baadhi ya madiwani wanampango wa kuhama chama hicho na kutimkia ccm.
Madiwani hao watatu wa makete waliotimkia CCM hivi
karibuni ni pamoja na Asifiwe Luvanda
aliyekuwa diwani wa kata ya Iwawa,Betrece Kyando aliyekuwa diwani wa viti
maalum kutoka tarafa ya Lupalilo na Efati Mbogela Mwipelele aliyekuwa diwani wa
kata ya Ipelele ambao wamesema wamehamia CCM bila shinikizo toka kwa mtu
yeyote.
0 Comments