TANGAZA NASI

header ads

Meya Jacob wa Ubungo akanusha kufukuzwa uanachama


Ndugu zangu watanzania,Nawaomba mpuuze habari inayozunguka mitandaoni kuwa nimefukuzwa Chama na ngazi yangu ya kata Ubungo.

Mimi sijawahi Kufukuzwa wala kujadiliwa au kupewa barua ya kufukuzwa Chama kwa ngazi yoyote ile ndani ya Chama Changu CHADEMA,Nimempigia Mkurugenzi Wa Manispaa ya Ubungo kumjulisha kuwa barua hiyo aliyopokea ni Fake na aipuuze

Na kiongozi waliyetumia Jina lake Kuwa ni katibu wa Chadema Ubungo,alishaachana na Maswala ya siasa na kwa sasa Ubungo ina katibu wa kata kwa Muda wa Miaka 3 Sasa.

na yeye ameshangazwa kuona barua hiyo mitandaoni,kesho tutakamilisha hatua ya kufikisha Barua rasmi ya Ashery Mlahangwa kwa mkurugenzi kumjilisa kuwa yeye si kiongozi wa kata Ubungo na kwamba ajawahi Kuandika Barua ya Namna hiyo.

Wanatutoa nje ya mchezo,tuachane na kupambana na Corona,tujadiliane mambo ya barua fake ambazo mtu kama mkurugenzi anaingizwa mkenge anashindwa kubaini kama ya kweli au si kweli.

Tuendelee Kujilinda na Corona Ndugu  zangu.

Post a Comment

0 Comments