Na Amiri kilagalila,Njombe
Madiwani watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wilayani
Makete mkoani Njombe,wamehama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi
CCM.
Madiwani hao ni miongoni mwa madiwani kutoka kata
saba zinazoongozwa na CHADEMA,hali inayofanya Chama hicho kubakiwa na kata nne
katika kata ishirini na tatu zilizopo wilayani Makete huku kata nyingine
zikiongozwa na CCM.
Akizungumza wakati akiwapokea madiwani hao,katibu wa
siasa na uenezi mkoa wa Njombe Ndg,Erasto Ngole amesema madiwani aliowapokea ni
pamoja na Asifiwe Luvanda aliyekuwa diwani wa kata ya Iwawa,Betrece Kyando
aliyekuwa diwani wa viti maalum kutoka tarafa ya Lupalilo na Efati Mbogela
Mwipelele aliyekuwa diwani wa kata ya Ipelele.
Ngole amewataka madiwani hao kuto kuogopa kusema
ukweli ndani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuwa Chama hicho chini ya Rais Dkt,John
Pombe Magufuli ndivyo kinavyotaka kwa kuzingatia taratibu,kanuni na sheria
kupitia katiba.
“Nyinyi mnaokuja usiogope kusema ukweli,moja iwe
moja na mbili iwe mbili,ndivyo CCM ya sasa inavyotaka na ndivyo mwenyekiti wetu
Magufuli alivyo,kwa hiyo njooni huku mje mshauri,mtembee na sisi, na zile tabia
zako ulizokuwa nazo CHADEMA ambazo wananchi wanazipenda endelea nazo ili
wananchi kwa tabia ile ile wakaendelee kuipenda CCM”Alisema Erasto Ngole.
Merry Mkoka ni katibu wa Jumuiya ya wanawake UWT
mkoa wa Njombe,amesema anaamini madiwani hao wamevutiwa na utekelezaji wa ilani
ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na ushirikiano mzuri baina ya Chama na serikali.
“Nimezungumza hivyo kwasababu ya ushirikiano mzuri na
upendo mzuri baina ya Chama na Serikali ndio maana nimeona DC wa Makete yuko
hapa leo”alisema Merry Mkoka
Naye Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Makete Ona Sukunala Nkwama amesema madiwani hao
hawajawahi kukasfu wala kukebehi Chama cha Mapinduzi huku wakitekeleza miradi
mingi kwenye kata zao,hivyo amewahakikishia ushirikiano wa hali ya juu ndani ya
CCM.
“Niwahakikishie Chama kitakuwa na ninyi na mtapata
ushirikiano wa hali ya juu wala hamtajutia maamuzi yenu hayo”
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya
ya Makete Ndg,Ignatio Mtawa amesema madiwani hao amekuwa nao zaidi ya miaka
minne kama mwenyekiti wao ndani ya baraza la madiwani,anawafahamu vizuri kwa
kuwa walikuwa ni wapinzani wa kweli kwa kujua wapi wapinge na kuunga mkono.
“Naomba nizungumze kwa wapinzani wote Tanzania,hawa
madiwani watatu kwenye baraza langu mimi niliwahesabu kuwa ni wapinzani wa
kweli kwa kuwa walikuwa wanajua wapi wapinge na wapi waunge mkono,kwa kweli
kenye sehemu ya kuunga mkono waliunga na kwenye sehemu ya kupinga walipinga
sasa yalipoisha ya kupinga ndio maana wamechukuwa uamuzi huu,hawa walikuwa
wanajenga hoja kwenye baraza vizuri sana na hakuna hoja yao niliyowahi kuona ni
ya kipuuzi”alisema Mtawa
Aidha mkuu wa wilaya ya Makete Bi,Veronika Kessy
amesema madiwani hao walikuwa mstari wa mbele kutekeleza Ilani katika maeneo
yao bila msuguano wowote,hivyo yuko tayari kuendelea kuwaongezea ulinzi hasa
katika kipindi hiki kwao.
“Mimi naona Madiwani hawa waliorudi Chama cha
Mapinduzi wote hawa ni CCM kwasabubu walikuwa mstari wa mbele katika kutekeleza
Ilani kwenye maeneo yao,kwa hiyo nasema hawa ni wenzetu walikuwa tu wamechepuka
kwa kwenda upande ule na leo wamerudi kutokana na heshima ya Mh.Rais”alisema
Veronika Kessy
Betrece Kyando, Asifiwe Luvanda na Efati Mbogela
Mwipelele ni madiwani waliohama Chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA,wamesema wamehama chama hicho bila shinikizo la mtu yeyote hivyo
wanaamini wapo watakao umia na watakao furahi,huku Betrece Kyando
akiwahakikishia Chama cha Mapinduzi kwenda kufanya kazi pasipo kusimama kwenye
maslahi ya mtu.
“Siku zote sijawahi simama kwenye maslahi ya mtu kwa
kuwa imani yangu ni kwamba Makete ni namba moja,na sitakuwa tayari kuto kufanya
yale yaliyonipasa ndani ya chama eti kwasababu ya maslahi ya mtu fulani Mwenezi
ukiskia nilikaidi ujue nilikuwa kinyume na anayenituma lakini kama anachonituma
ni sahihi kwa maslahi ya umma nitafanya sawa sawa na nilivyotumwa”alisema
Betrece.
Madiwani watatu kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema waliohamia Chama cha Mapinduzi wakisomewa kiapo cha utii na uongzo wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe
Katikati katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole akionyesha Kadi ya mmoja wa madiwani ya CHADEMA iliyolejewa na mmoja wa madiwani waliohama chama hicho.
Katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole akizungumza na viongozi wa CCM mara baada ya kuwapokea madiwani wapya kutoka CHADEMA
Katibu wa UWT mkoa wa Njombe Merry Mkoka akifurahi wakati wa kuwakaribisha katika chama hicho madiwani wapya kutoka CHADEMA.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ona Sukunala Nkwama akiwapa neon la faraja madiwani hao mara baada ya kupokelewa na Chama cha Mapinduzi.
Mkuu wa wilaya ya Makete Bi,Veronika Kessy akitoa ufafanuzi namna madiwani wa Chadema waliohamia CCM ambavyo walikuwa wakitoa ushirikaino katika Maendeleo ya kata zao.
Madiwani watatu kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema waliohamia Chama cha Mapinduzi wakisomewa kiapo cha utii na uongzo wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe
Katikati katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole akionyesha Kadi ya mmoja wa madiwani ya CHADEMA iliyolejewa na mmoja wa madiwani waliohama chama hicho.
Katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa Njombe Erasto Ngole akizungumza na viongozi wa CCM mara baada ya kuwapokea madiwani wapya kutoka CHADEMA
Katibu wa UWT mkoa wa Njombe Merry Mkoka akifurahi wakati wa kuwakaribisha katika chama hicho madiwani wapya kutoka CHADEMA.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ona Sukunala Nkwama akiwapa neon la faraja madiwani hao mara baada ya kupokelewa na Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete
Ndg,Ignatio Mtawa akikili namna madiwani hao walivyokuwa na uwezo mkubwa katika
kujenga hoja ndani ya baraza la madiwani.
Mkuu wa wilaya ya Makete Bi,Veronika Kessy akitoa ufafanuzi namna madiwani wa Chadema waliohamia CCM ambavyo walikuwa wakitoa ushirikaino katika Maendeleo ya kata zao.
Betrece Kyando aliyekuwa diwani wa viti maalum
kutoka tarafa ya Lupalilo akifafanua namna ambavyo amekuwa akishirikiana na
madiwani wa kada zote pamoja na serikali ndani ya baraza la madiwani wilaya ya
Makete.
0 Comments