Misikiti kote nchini Iran imepangiwa kufunguliwa Jumanne hatua
inayowadia licha ya kwamba baadhi ya maeneo bado yanaathirika vibaya na
janga la virusi vya corona.
Hatua hiyo ni miongoni mwa mikakati ya serikali ya kuongeza masharti
iliyokuwa imeweka kama njia moja ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.
Uamuzi huo unawadia baada ya majadiliano na wizara ya Afya.
Aidha ambacho bado hakijaeleweka ni kwamba baadhi ya maeneo nchini humo bado yana kiwango cha juu cha maambukizi.
Kufikia Jumapili eneo la kusini mashariki mwa Iran lilikuwa limeweka
chini kanuni ya kusalia ndani kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi
vya corona.
Ijumaa iliyopita, mikusanyiko kwasababu ya sala ilikuwa imerejea katika
miji 180 yenye kuonekana kuwa na kiwango cha chini cha hatari ya kupata
maambukizi baada ya kukatizwa kwa miezi miwili kulingana na kituo cha
habari cha taifa.
Kurejelelewa kwa sala ya Ijumaa bado kumepigwa marufuku katika mji wa
Tehran na miji mingine mikubwa baada ya kufunguliwa tena kwa misikiti
132 Jumatatu iliyopita katika maeneo ambayo hayakuathirika na virusi vya
corona.
Aidha shule zinatarajiwa kufunguliwa wiki ijayo, Rais Hassan Rouhani alisema Jumapili, kulingana na tovuti rasmi ya rais.
Iran tayari imeondoa marufuku ya kusafiri baina ya miji na majengo ya
kibiashara huku shughuli za kibiashara zikiwa zimerejelelewa.
Iran, moja ya maeneo ya Mashariki ya Kati yaliyoathirika vibaya na
virusi vipya vya corona imeanza kulegeza masharti na kurejelelea maisha
ya kawaida ili kufufua uchumi ambao tayari unakumbana na vikwazo vya
Marekani.
Hata hivyo maafisa wa afya wameonya kwamba kulegeza masharti kunaweza
kusababisha wimbi jengine la maambukizi ya virusi vya corona.
0 Comments