Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof Palamagamba Kabudi amezitaka Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuimarisha ushirikiano na umoja wakati huu wa kuenea kwa janga la Virusi vya Corona huku bidhaa na huduma muhimu zinazovuka mipaka baina ya nchi na zikiendelea kutolewa.
Prof.
Kabudi amesema hayo jijini Dar es salaam wakati akifungua Mkutano wa
Baraza la Mawaziri wa SADC kwa njia ya Video katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Nawaomba
Nchi zote Wanachama wa SADC tuimarishe umoja na mshikamano wetu wakati
huu wa kuenea kwa janga la Virusi vya Corona, huku bidhaa na huduma
muhimu zinazovuka mipaka baina ya nchi nan chi zikiendelea kutolewa, huu
ni wakati wa kuepuka vitendo vya kujitenga na kuongeza mashauriano
baina ya nchi,” amesema.
Aidh
Mhe Waziri ameziomba Nchi za SADC kuwapa heshima na kuthamini utu wa
madereva wanaosafirisha bidhaa na huduma muhimu kuvuka mipaka ya nchi
kwa wakati huu ambao ugonjwa wa corona umeenea katika nchi wanachama.
Amesema
Nchi wanachama zinapaswa kuchukua hatua za kukabiliana na ueneaji wa
virusi vya Corona bila ya kuwanyanyapaa madereva na kuwachukulia kama
watu wanaosambaza virusi hivyo na kuongeza kuwa madereva hao wanapaswa
kupewa heshima stahiki kama binadamu wengine na kuwashukuru kutokana na
hatari wanayochukua ya kusafirisha mizigo na huduma wakati huu wa kuenea
kwa janga hilo.
“Madereva
wetu wamevunjika moyo kwa sababu wanaonekana kama wao ndio wanaosambaza
virusi vya Corona na sio askari wazuri ambao wanatoa huduma ya
kusafirisha huduma na biidhaa muhimu wakati huu wa mlipuko, katika nchi
za jumuiya,”
Ameziomba
nchi za SADC kuwapa heshima na kuthamini utu wa madereva hao huku
zikiendelea kuchukua tahadhari za kupambana na janga la virusi vya
corona na kuongeza kuwa umoja wetu ni muhimu sana kwa wakati huu.
“Naziomba
nchi zetu tuwape heshima na kuthamini utu wa madereva hao na kuwapa
heshima wanayostahili huku tukiendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa
na wataalamu wa afya katika kukabiliana na janga hilo,” alisema.
Prof.
Kabudi amesema janga la COVID 19 linaonekana kama halitoisha ndani ya
muda mfupi na nchi za ukanda wa SADC lazima ziishi kwa kufuata mifumo
salama katika biashara na usafirishaji wa huduma na bidhaa ili kupata
ukuaji wa uchumi na kuondoa umasikini huku tukiwa bado tunakabiliana na
janga hili la ueneaji wa virusi vya corona.
Amesema
wakati hatua za kukabiliana na janga la Corona zikiendelea kuchukuliwa
nchi za SADC lazima zikumbuke dhumuni la utangamano miongoni mwa nchi
wanachama ambalo ni kuboresha ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi na
hivyo kutowaangusha waanzilishi wa Jumuiya ya SADC.
Amesema
ufanyaji wa biashara baina ya nchi na nchi ndani ya SADC uko chini ya
asilimia 20 hali ambayo inazuia nchi wanachama kuona ukuaji wa uchumi
wake na kuongeza kuwa janga la corona lichukuliwe kama chachu ya
kuongeza juhudi za kuinua kiwango cha ufanyaji biashara baina ya nchi na
nchi kupitia utekelezajia wa Protokali ya SADC katika biashara ya 2005
na uanzishwaji wa eneo huru la biashara la SADC.
Ujumbe
wa Tanzania ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwele na Waziri wa Maliasilia na Utalii Dkt.
Hamisi Kigwangala.

0 Comments