Na,Tiganya Vincent
IDARA ya Afya ya Halmashauri ya
Wilaya ya Sikonge imeagizwa kuhamia katika jengo la Utawala katika Hospitali ya
Wilaya hiyo na waanze kutoa huduma ya watibabu kwa wananchi.
Kauli hiyo imeolewa jana na Mkuu wa
Wilaya ya Sikonge Peres Magiri wakati akitoa salamu za Serikali katika Kikao
cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu
Alisema wakati wakiendelea kusubiri vifaa
tiba na vifaa vingine kwa ajili ya Hospitali hiyo ya Wilaya ni vema wakaanza na
utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa nje.
Magiri aliutaka uongozi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge kutoa walau sehemu ya mapato yake ya ndani kwa
ajili ya kujenga vyoo ili majengo yote muhimu ya awali yawepo na huduma zianze.
Alisema wanaweza kuanza kutoa huduma
kama zile zinazotolewa kwa kiwango cha Zahanati cha kuanzia walau asubuhi hadi
jioni kila siku.
Magiri alisema hatua hiyo
itawasaidia wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo wasipate shida ya kuembea
umbali mrefu kutafuta huduma kupima malaria na magonjwa mengine.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Peter Nzalalila alisema majengo ya Hospitali
ya Wilaya hiyo hayakujengwa kutazamwa bali kutoa huduma kwa wananchi.
Alisema ni vema Mejimenti ya
Halmashauri hiyo ikaangalia uwezekano wa kuanza kutoa huduma za matatibu katika
eneo hilo kwa kutumia watalaamu waliopo wakati wakisubiri kupata wengine.

0 Comments