Na Amiri kilagalila,Njombe
Serikali wilayani Njombe imeagiza wafanyabishara wa
Sukari wilayani humo kuzingatia bei elekezi iliyopangwa na serikali kufuatwa
katika mkoa huo ili kudhibidi mlipuko na wizi unaofanywa na baadhi ya
wafanyabiashara.
Ili kudhibiti kasi ya ongezeko la bei ya sukari
nchini serikali imepanga bei ya sukari kwa kila mkoa kulingana na mazingira na
mahitaji kwa kuzingatia sherikali sheria ya Sukari No 26 ya Mwaka 2001(Cap. 251) chini ya
kifungu cha 11A ambayo imeutaka mkoa huo kuuza sukari kwa bei ya jumla mfuko wa
kg 50 jumla kwa shilingi 135000 ambapo kg 1 itauzwa shilingi 2700 huku bei ya
reja reja ikiagiza kuuzwa shilingi 2900
Akitoa agizo hilo alipokutana na wafanyabiashara wa
sukari mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri anasema wafanyabiashara wamekuwa
wakijipangia bei kwa matakwa yao jambo ambalo linawaumiza wananchi na kwamba
kuanzia sasa watapaswa kuzingatia bei elekezi bila kujali mazingira ya
upatikanaji wake.
Aidha Dc Msafiri amesema ili kuhakikisha takwa hilo
la kisheria linatekelezwa ni muda wowote timu ya ulinzi na usalama itaingia
mtaani kufanya ukaguzi kama bei hizo zinafuatwa.
“Na kamati yangu ya usalama,itanisaidia kuhakikisha
kwamba bei hizi tulizoletewa kuhakikisha tunazitekeleza kuanzia sasa”alisema
Ruth Msafiri
Baadhi ya wafanyabiashara ambao wameshiriki katika
kikao hicho akiwemo Rodrick Sanga na Harid Mbilinyi wanasema wamepokea agizo
hilo lakini wanaiomba serikali kuwasaidia kupata sukari kwa kuwa mkoa huo
umeishiwa kabisa sukari.
“Sukari mpaka tunavyoongea hivi Njombe hamna,na
muuzaji Dar es Salaam ni mtu mmoja,sawa tumepokea hilo lakini sukari hatuna
tunaomba tupate maelekezo labda tutaipata kwa nani” Alisema Rodrick Sanga
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya amepiga
marufuku kwa wafanyabishara ambao watathubutu kuficha sukari ili waweze kuja
kuuza baadae kwa faida zaidi na kwamba hadi sasa bei ya sukari imekuwa ikiuzwa
zaidi ya elfu 3100.
“Serikali inajua njia zote inako tokea Sukari,lakini
kinyume na bei hii mtu asinunue sukari,na sisi wakati wowote ule tutajipanga
kuhakikisha tunakagua uwepo wa sukari”alisema Msafiri
Wakati serikali ikipanga bei ya shilingi elfu 2900
ya sukari katika mkoa wa Njombe ,mkoa wa Iringa ni shilingi 2900, Mbeya 3000
huku Katavi na Ruvuma zikipewa shilingi 3200.
0 Comments