Wizara ya Maliasili na Utalii imewasilisha bajeti yake ya
mwaka 2020/2021 huku ikiweka bayana athari zitakazotokana na uwepo wa ugonjwa
wa Corona unaosababishwa na virusi vya homa kali ya mapafu (COVID 19) ikiwemo
kushuka kwa makusanyo ya taasisi zilizochini ya wizara hiyo kwa asilimia 75.
Taasisi hizo ni Shirika la Hifadhi la Taifa(TANAPA),mamlaka
ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA),Mamlaka ya usimamizi wa unyamapori
Tanzania(TAWA) na wakala wa misitu Tanzania(TFS).
Akiwasilisha bajeti Bungeni jijini Dodoma,waziri wa
wizara hiyo Dokta Hamisi Kigwangalla amesema endapo hali itatulia mwezi Oktoba
2020 mapato yatokanayo na utalii yanatarajiwa kushuka kutoka shilingi trilioni
2.6 zilizotarajiwa hadi shilingi Bilioni 598.
0 Comments