Wilaya ya bahi Mkoani Dodoma imedhamiria kuwasaidia wafugaji Kufuatia
hivi karibuni kuanza kwa mchakato wa Ujenzi wa kiwanda cha Kuchakata
ngozi ili kuwawezesha kujikwamua kiuchumi hatua itakayochochea kufikia
uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.
Mbunge wa wilaya ya Bahi Bw,Omary Badwell amesema kuwa moja ya
changamoto ambayo imewakabili kwa muda mrefu wafungaji ni ukosefu wa kiwanda
cha kuchakata ngozi katika wilaya hiyo ambayo ni miongoni mwa wilaya zenye
mifugo mingi Mkoani Dodoma.
Bw,Omary ameongeza kuwa kufuatia changamoto hiyo wilaya ya bahi
imefanya utaratibu wa kuhakikisha inapata fedha za ujenzi wa kiwanda cha
kachakata Ngozi.
Aidha Bw Omary amebainisha kuwa kipindi cha nyuma ngozi zilikuwa
hazina thamani kwani ailikuwa zinatumika kulalia pamoja na kuzitupa hivyo
wilaya hiyo imeona ngozi ni moja ya fursa amabyo itawapatia ajira vijana na
kujikwamua kiuchumi.
Kwa mujibu wa Chama Cha Kusindika Ngozi Tanzania katika taarifa yake mwaka 2017 kilieleza
kuwa kuna ukosefu wa ngozi unaofikia zaidi ya asilimia 80, na ngozi
inayopatikana ni chini ya asilimia 20 kutokana viwanda vilivyopo kuwa na uwezo
mdogo wa kusindika ngozi.
0 Comments