TANGAZA NASI

header ads

Ludewa kwa zidi kunoga,mkataba wa mamilioni wasainiwa kufikisha umeme mwambao wa ziwa Nyasa



Wakandarasi kutoka kampuni ya JV Mufindi Power Services Ltd wakisaini mkataba wa usambazaji umeme wilayani Ludewa huku pembeni afisa kutoka REA akifuatilia hatua za kusaini mkataba huo.




Mkuu wa wilaya ya Ludewa Adrea Tsere mbele akishuhudia utiani wa saini kwa ajili ya kusambaza umeme baadhi ya vijiji vya Mwambao wilayani Ludewa.




Kushoto Mkuu wa wilaya ya Ludewa Adrea Tsere akipokea mkataba wa usambazaji umeme kutoka kwa mkandarasi JV Mufindi Power Services Ltd wa usambazaji umeme vijiji vinne vya Mwambao.




Merkion Ndofi mkurugenzi wa rasirimali watu na utawala REA amesema mara baada ya utiaji saini akifafanua namna mkataba huo utakavyotekelezwa na kutakiwa kukamilika tarehe 30 Juni 2020.





Baadhi ya maafisa kutoka Tanesco,halmashauri ya wilaya ya Ludewa wakiwa makini kufuatilia utiaji wa saini kwa ajili ya usambazaji umeme vijijini.



Merkion Ndofi mkurugenzi wa rasirimali watu na utawala REA akiwaeleza wanannchi wa Makonde kujipanga na kuchangamkia fursa ya kufikiwa na umeme.




Wananchi wa kijiji cha Makonde wakifurahi taarifa za kufikiwa na umeme pamoja na kukabidhiwa mkandarasi atakayefikisha umeme katika kijiji hicho.


Na Amiri kilagalila,Njombe

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umesainiana mkataba wenye thamani ya zaidi ya mil 920 na kampuni ya JV Mufindi Power Services Ltd wa kusabambaza umeme katika vijiji 4 vya tarafa ya mwambao wa ziwa Nyasa wilayani Ludewa mkoani Njombe ambavyo vimekuwa na changamoto hiyo kabla na baada ya uhuru .

Akizungumza mara baada ya kupokea  mkataba huo,mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrew Tsere amesema serikali imedhamilia kufikisha nishati ya umeme katika vijiji vyote wilayani humo na kumtaka mkandarasi kutekeleza mradi huo kwa mujibu wa Mkataba kwa kuwa ana imani unakwenda kubadilisha maisha ya wavuvi.

“Kwa hiyo kila siku nitakuwa narejea mkataba huu kama ulivyoandikwa na kama unatekelezwa tulivyokubaliana hivyo wakandarasi wajiandae kuweka mpango wa utekelezaji wa mkataba huu,na sisi tutawapa ulinzi na usalama kwa kuwa sina mashaka kwamba umeme huu utabadilisha maisha ya wavuvi na wataongeza thamani ya maisha yao,na wakisi wale watapata ajira kupitia wakandarasi hawa”alisema Tsere

Tsere amesema wananchi watakaofikiwa na huduma ya umeme ni 583 wa kutoka vijiji vinne vya Mkwimbili,Nsisi,Lifuma na Makonde vilivyopo tarafa ya Mwambao huku mkataba huo ukiambatanisha shughuli za uwekaji wa HT Scope Kilomita 18.1, LV Scope kilomita 11.8,Transfoma 8 huku mkataba huo ukighalimu Milioni mia tisa ishirini na moja,mia tano elfu arobaini na tisa na mia nane arobaini na nne nukta sita nane.

Mbali na kuzungumzia matokeo chanya ya usongezaji wa huduma ya umeme katika vijiji vya mwambao Dc Tsere pia amemuonya mkandarasi kumaliza kazi katika muda uliopangwa vinginevyo atawekwa ROCK UP na kumtaka mkandarasi kutafuta nyumba ili kukaa eneo la mradi.

Nae Merkion Ndofi mkurugenzi wa rasirimali watu na utawala REA amesema mpaka sasa wilayani Ludewa vijiji vipya ambavyo vimefikiwa na umeme ni 16 lakini jumla ya vijiji 63 vimepata umeme wa REA NA kubakia vijiji 14 kati ya vijiji 77 vya wilaya ya Ludewa huku vijiji hivyo 14 vilivyobaki vikiingwiza REA awamu ya pili.

Aidha bwana Merkion Ndofi amesema mkataba huo ni sehemu ya mkataba mkuu wa utoaji umeme mkaoni Njombe na wilaya ya Ludewa unaotakiwa kukamilika  tarehe 30 Juni 2020.

“Mkataba huu ni sehemu ya mkataba mkuu wa utojai umeme ambao unatakiwa kukamilika tarehe 30 Juni Mwaka huu 2020 pamoja na mikataba yote ya umeme wa REA nchi nzima inatakiwa kuwa umekamilika,kwa hiyo Mkandarasi anatakiwa atueleze atafanyaje kazi na hayo maelezo yatathibitishwa na Tanesco pamoja na Rea”alisema Ndofi

Ujio wa mradi huo umepokelewa kwa mikono miwili na wakazi wa vijiji hivyo vya pembezoni mwa ziwa Nyasa na kuahidi kushirikiana na watalaamu kutekeleza mradi huo ambao wanautaja kuja kubadili maisha yao.

“Watu wakienda kuvua samaki wanakosa soko kwasabau umeme hauo ila tukifikiwa na umeme watu watazihifadhi vizuri ili zisiweze kuharibika kwa muda mfupi”alisema mmoja wa wananchi


Post a Comment

0 Comments