Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kwa uongozi imara katika kuhakikisha Huduma za Matibabu ya Dharura zinashushwa ngazi ya Hospitali za Wilaya.
Dkt. Jakaya Kikwete ametoa pongezi hizo alipohudhuria hafla ya makabidhiano ya ramani katika eneo la ujenzi wa jengo la Huduma za Matibabu ya Dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze- Msoga kwa Mkandarasi.
“Tulipokuwa na wazo la kujenga Hospitali yetu hii mpya tulizungumza na viongozi wa ABBOT pamoja na Dkt. Dorothy Gwajima wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, alisatusaidia sana”ameshukuru Mhe. Kikwete.
Hospitali ya Chalinze, Msoga inakuwa Hospitali ya kwanza ya Wilaya kuwa na Huduma za matibabu ya dharura nchini huku ikiwa kwenye eneo ambalo ni njia panda ya kuelekea Mikoa ya Kaskazini na Nyanda za Kati ya nchi na Nyanda za Juu Kusini eneo ambali halina huduma za dharura kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji wa huduma za haraka hususani wale wanaopata ajali.
0 Comments