TANGAZA NASI

header ads

Wachezaji England kupimwa Corona kabla ya mchezo


MTENDAJI Mkuu wa Chama cha Makocha wa Ligi England, Richard Bevan, amesema msimu wa soka nchini humo hautaendelea kama wachezaji wote hawatapimwa Corona. 

Kauli hiyo inawagusa wachezaji wote kuanzia Ligi Kuu England maarufu Premier ambapo Mtanzania, Mbwana Samatta anaichezea Aston Villa, hadi ligi za chini.


Bevan ameiambia BBC Sport kuwa: “Suala la kufanyiwa vipimo ni muhimu kwanza kabla ya mambo mengine kuendelea.” 

Hivi sasa ligi mbali mbali duniani zimesimama kutokana na janga la Virusi vya Corona.Bosi huyo wa makocha amesema anachoangalia kwa sasa ni kuzungumza na viongozi wa soka nchini humo kuona namna gani msimu utaendelea.

Post a Comment

0 Comments