Msanii wa muziki Bongo, Dudubaya ameitwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa ajili ya mahojiano.

Katika barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza imesema baraza limesikitishwa na kauli zisizokuwa na maadili wala staha alizoweza kuzitoa msanii Dudubaya bila kuzingatia maadili mema katika jamii.

Dudubaya anatakiwa kuripoti Jumanne ya tarehe 14, 2020 kufika ofisi za baraza hilo zilizopo Ilala Sharif Shamba, Dar es Salaam, Tanzania.