Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia kusoma hukumu ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe Mei 29 mwaka huu huku ikitoa hati ya kumkamata kwa kutohudhuria kwenye shauri lake bila taarifa.
Amri
hiyo ya kumkamata Zitto ambaye anakabiliwa na mashtaka matatu ya
uchochezi, ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.
Hukumu
ilipangwa kusomwa Mei 29 mwaka huu, baada ya upande wa mashtaka na
utetezi kufunga ushahidi na kuwasilisha majumuisho ya mwisho kwa
kuirahisishia mahakama kufikia uamuzi.
Wakili
wa Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, alidai shauri lilitajwa kwa ajili ya
kupanga tarehe ya hukumu ambapo mshtakiwa hakuwepo na hakuna taarifa
kuhusu kushindwa kufika kwake mahakamani.
”Mheshimiwa
Hakimu mshitakiwa hayupo na muda wa mahakama unafahamika ni saa tatu
asubuhi na hakuna taarifa yoyote ingawa mshtakiwa hana tabia ya
kushindwa kufika mahakamani,” alidai.
Baada
ya kudai hayo, Hakimu Shaidi alisema hati ya kukamatwa itolewe, kesi
iliahirishwa hadi Mei 29, mwaka huu kwa ajili ya hukumu.
Katika
kesi hiyo inadaiwa Oktoba 28 mwaka juzi, Zitto aliitisha mkutano wa
waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Makao Makuu ya ACT Wazalendo,
akiwa na lengo la kuleta chuki kwa raia wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kinyume na sheria na kwamba alitoa maneno ya uchochezi dhidi ya
Jeshi la Polisi.
0 Comments