Spika wa Bunge Job Ndugai, amesema kuwa kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, haimbabaishi na chochote kwa kuwa kila jambo lao wanaweka upinzani na Wabunge ni timu moja na yeye ameamrisha timu yake tu bila kushirikisha wenzake, hivyo Wabunge wa CCM watabaki na kuendeshesha Bunge.
"Sisi halitushangazi hawa wenzetu kila jambo lazima waweke upinzani hata kama ni janga, Wabunge ni timu moja hauwezi kuamrisha tu wachezaji wako kwamba tokeni bila kuzungumza na wenzako, Wabunge wa CHADEMA wana bahati mbaya sana kazi yao ni kuamrishwa tu kama watoto wa Primary vile na wanalalamika kimya kimya sana kwangu" amesema Spika Ndugai.
Aidha Spika Ndugai alizungumzia suala la kupokea ushauri wa Mbowe "Wala siko tayari tena, yeye aendelee tu na Methodology zake kwa sababu muda mfupi ujao tutamaliza Bunge kwa kuzingatia tatizo la Corona na toka tumeanza tumezingatia na tumebadilisha mambo mengi sana".
0 Comments