Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya aliyekuwa mchungaji wa kanisa la Mikocheni B Assemblies of God na mbunge wa viti maalum, mchungaji Getrude Rwakatare inaratibu mazishi ya mbunge huyo aliyefariki dunia alfajiri leo Jumatatu Aprili 20.
Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema hayo katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge ambapo mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Akizungumzia kifo cha Mchungaji Rwakatare, Spika Ndugai amesema; “Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Rwakatare.
“Natoa pole kwa wafiwa wote wakiwamo familia ya marehemu, ndugu, jamaa, waheshimiwa wabunge na waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Ndugai.
Chanzo:Mpekuzi blog
0 Comments