ZANA Coulibaly, raia wa Ivory Coast amesema kuwa yupo tayari kurejea Bngo kukipiga ndani ya Yanga iwapo watahitaji huduma yake.
Beki
huyo alidumu Simba kwa miezi tisa kabla ya kuondoka na kujiunga na AS
Vita ya DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili katika michuano ya
kimataifa amefanikiwa kucheza mechi tatu pekee msimu huu.
Coulibaly
amesema kuwa moja kati ya sehemu ambazo hawezi kuzisahau kirahisi ni
Tanzania na yupo tayari kurejea kwa kujiunga na timu yoyote zikiwemo
Azam na Yanga kutokana na ukarimu wa watu wake.
“Tanzania
kiukweli nilikuwa na furaha kwa sababu watu wake ni wakarimu na
wanawajali wengine, ukiangalia katika mechi mashabiki wanajitokeza kwa
wingi na wakati wote wanashangilia kitu ambacho ni nadra kukiona katika
mataifa mengine ya Afrika, bado nawakumbuka sana.
“Natamani
kuona narudi tena huko kucheza haijalishi ni timu gani iwe kama Azam au
hata Yanga wakinihitaji nitakuwa tayari kurejea,” amesema Coulibaly.
0 Comments