Na,Maiko Luoga Iringa
Waumini wa dini ya kikristo nchini wameshauriwa kuongeza kasi ya maombi wawapo kwenye nyumba za ibada au majumbani mwao ili mwenyezi Mungu aweze kusikia maombi hayo hatimae kutoa hitimisho ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID-19).
Wito huo umetolewa na askofu wa kanisa Anglikana Tanzania fayosisi ya Ruaha mkoani Iringa Dkt, Joseph Mgomi wakati akiendesha Ibada ya kufufuka na kupaa mbinguni kwa Yesu kristo (Pasaka) iliyofanyika kwenye kanisa kuu la dayosisi hiyo Kristo Mfalme Iringa Mjini.
Licha ya kuwakumbusha waumini wa kanisa hilo maisha ya Yesu Kristo alipokuwa duniani zaidi ya miaka 2000 iliyopita, askofu Mgomi amewataka Waumini hao kutumia nafasi hiyo kupaza sauti za maombi ili mwafaka wa Janga hilo la Kidunia uweze kupatikana.
“Tuwapo Kanisani au Nyumbani tunatakiwa kuongeza kasi ya Maombi kwa Mwenyezi Mungu ili atuepushe na Janga hili la Kidunia la Homa ya CORONA au COVID-19 tunaamini kupitia maombi hakuna linaloshindikana mbele za Mungu” Askofu Dkt, Joseph Mgomi.
Athanas Ndalu katibu wa kanisa kuu Anglikana Iringa Mjini na Asheri Sadala mzee wa kanisa hilo wamesema kanisa linaendelea kutekeleza maagizo ya kitaalamu yanayotolewa na wizara ya afya nchini, huku wakishauri Waumini wa Kanisa hilo na Watanzania wote kuzingatia maagizo ya Wataalamu wa afya.
“Tunatakiwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wetu wa afya chini ya waziri Ummy Mwalimu ikiwemo kuchukua tahadhari wewe mwenyewe binafsi na familia yako kwa kuzingatia usafi na maelezo mengine ili kujikinga na Janga hili”Athanas Ndalu.
Baadhi ya waumini walioshiriki Ibada Kanisani hapo akiwemo Bi, Sara Ng’akamo na Bw, Saimoni Kanyara wamesema Nyumba za Ibada bado zina umuhimu mkubwa katika kipindi hiki kwaajili ya kumwomba Mungu ili aweze kuliepusha Taifa na Dunia kwa ujumla dhidi ya Janga la CORONA ambalo limekuwa changamoto kubwa Dunia kote.
“Sisi tunaamini kwa Mungu hakuna kinachoshindikana ndio maana hatujakata Tamaa ya kuja kwenye Nyumba za Ibada na kupaza sauti za Maombi ili Janga hili kwa msaada wa Mungu lisiendelee kututesa Watanzania na Dunia” Sara Ng’akamo.
Ili kujikinga na homa kali ya mapafu inayotokana na virusi vya CORONA au COVID-19 uongozi wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Ruaha chini ya Askofu wake Dkt, Joseph Mgomi umeendelea kutoa maagizo kwa Wachungaji na waumini wa mitaa ya dayosisi hiyo kuhakikisha wanazingatia kanuni zote za kujikinga na homa hiyo
0 Comments