TANGAZA NASI

header ads

Amber Lulu afunguka Corona ilivyoathiri maisha ya wasanii



Mwimbaji Amber Lulu amesema kwa kipindi hiki ambacho wasanii hawafanyi show,hali zao za kiuchumi sio nzuri sana ukizingatia wengi wao hawakujiandaa na jambo hilo.

Ikumbukwe tangu kuandikishwa kisa cha kwanza cha mgonjwa wa corona nchini, serikali ilipiga marufuku mikusanyiko isiyo ya lazima kama kwenye michezo na matamasha ya muziki.

Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM, Amber Lulu amesema kwa sasa hana kazi yoyote zaidi ya kukaa nyumbani labda na mara chache kwenda studio kurekodi.

“Sasa hivi hamna show, hamna ile mitoko unaenda unakutana na mtu anakupa hela, yaani wale Ma-slay queen kama mimi tunapata tabu sana,”alisema na kuendelea.

“Yeah tunafanya shughuli nyingine nje ya muziki lakini sio kivile sana,” aliongeza Amber Lulu.

Ikumbukwe Amber Lulu alijizolea umaarufu mkubwa kipindi akiwa video vixen kabla ya kuingia kwenye muziki.

Amber Lulu ndiye video vixen wa kwanza kwa video yake kuweza kufikisha watazamaji (views) zaidi ya Milioni 1 kwenye mtandao wa YouTube kupitia wimbo wake unaokwenda kwa jina la Jini Kisirani.

Post a Comment

0 Comments