TANGAZA NASI

header ads

Mkuu wa wilaya ya Tanga ayataja maeneo yenye madanguro, atoa maelekezo



 Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa, ameyataja maeneo yanayotumika kama biashara ya madanguro ambapo ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kwamba biashara hiyo kwenye maeneo hayo inakoma mara moja. 

Agizo hilo amelitoa kwenye kikao cha baraza la madiwani wa hlamashairi ya jiji la Tanga ambapo Mgandilwa ameyataja maeneo hayo kuwa ni eneo la Sabasaba na barabara ya Uhuru na kusema kuwa wanaofanya biashara kwenye maeneo hayo watafute miji mingine. 

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo, amewataka wakuu wa idara kuheshimu maamuzi yanayofanywa na baraza la madiwani ili kuepukana na migongano isiyokuwa ya lazima inayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo kwenye jiji hilo. 

Post a Comment

0 Comments