TANGAZA NASI

header ads

Wadau waipa changamoto Brela kupambana na wapiga dili

 




Na Amiri Kilagalila,Njombe


Wadau na wafanyabiashara mkoani Njombe wenye uhitaji mkubwa wa huduma kutoka kwa wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela),wametoa wito kwa wakala kuongeza kasi ya kutoa elimu pamoja na kuifikia jamii ili kupunguza hatari ya wananchi wanaoingia ghalama kubwa kusajili kampuni zao kwa watu mitaani.


Wito huo umetolewa na wadau mbali mbali katika semina ya wakala wa usajili Biashara na Leseni {BRELA} katika mkutano wa wadau uliofanyika katika ukumbi wa Sido mjini Njombe kwa lengo la kuelimisha zaidi malengo ya Brela pamoja na huduma hizo za usajili ambazo kwa sasa mtu yeyote anaweza kutumia simu yake ya kiganjani inayotumia intaneti kusajili kampuni,leseni za biashara pamoja na huduma yeyote inayotolewa na Brela.



Baadhi ya wadau waliohudhuria katika mkutano huo akiwemo Frenk Msigwa na bwana Stiven Mlimbila wamesema semina waliopewa imewasaidia kutambua umuhimu wa kusajili jina la biashara huku wakiwaomba watu Brela wasiwe watu wa kukaa tu ofisini bali wajenge utaratibu wa kuwatembelea wajasiriamali na kuwapa elimu.


“Hii semina ya leo imenisaidia vitu vingi sana kwasababu kuna baadhi ya vitu tulikuwa tunapata Changamoto ikiwemo namna ya kumiliki kampuni,na ni changamoto zipi unatakiwa utatuliwe na nani na ukizingatia wakati mwingene utakuta mtu anataka kufungua kampuni basi itakulazimu kutumia watu ambao wamekuwa wakidai ghalama nyingi”alisema Stiven Mlimbila


Wadau hao wametaka watumishi wa Brela kuto kukaa ofisini “Hasa katika eneo la uvumbuzi nashauri Brela wasikae ofisini na kusubiri wafuatwe,wao wafaute watu kwa kuwa wavumbuzi Tanzania ni wengi lakini teknolojia zetu zinaibwa na wazungu”alisema mdau mwingine.


Wataalamu kutoaka wakala huyo wamekili kuanza kufanyia kazi maoni hayo ili kupunguza changamoto ya ulaghai kwa wateja wanaolazimika wakati mwingine kulipa mpaka shilingi 150,000 kwa watu mitaani ili wasajiliwe kampuni huku wakitoa rai kwa wafanyabiashara mkoani Njombe kusajili majina ya biashara zao ili kuepukana na kuibiwa majina ya biashara zao na baadhi ya watu wasio waaminifu ili  kuwasaidia kupata ulinzi wa kisheria na serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambapo halitatumiwa na mtu mwingine.



Swalehe Yahaya msajili msaidizi wa Wakala wa usajili Biashara na Leseni {BRELA} ametoa wito huo na kubainisha kuwa watu wengi wamekuwa wakiibiwa majina kwa sababu ya kutoyasajili.


“Tunawasisitiza na kuwaomba msajili majina ya biashara kwani yana faida kubwa sana,unaposajili jina la biashara kwanza unapata ulinzi wa kisheria kwa kuwa na cheti cha usaili wa jina la biashara yako na jina hilo linalindwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”alisema Swalehe Yahaya


Rajabu Chambega ni afisa Leseni  kutoka Brela amesema kuwa ni jambo la mhimu kwa mfanyabiashara kuwa na leseni ya Biashara kwakua kufanya biashara bila lesen ni kosa la jinai na pia itasababisha  kuto tambulika kisheria.


“Leseni ya biashara ni kibali maalumu anachopewa mfanyabiashara anapotaka kufanya biashara hapa nchini kwa maana hiyo kufanya biashara pasipo kuwa na leseni ni kosa la jinai.lakini pia faida nyingine ya kuwa na leseni ni kwamba hauwezi kwenda benk ukapewa leseni ya kibiashara pasipokuwa na uthibitisho kwamba wewe ni mfanyabiashara”alisema Rajabu Chambenga


Post a Comment

0 Comments