Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wanachana wa Chama cha Demokrasia na maendeleo
CHADEMA mkoani Njombe wametakiwa kuendelea kushirikiana ili kukijenga
chama hicho hasa katika kipindi hiki ambacho wanajenga ofisi ya jimbo la
makambako.
Akizungumza na wanachama wa chama hicho jimbo la Makambako
mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) Taifa JOHN PAMBALU amesema kuwa
licha ya changamoto wanazokutana nazo kisiasa bado wapo imara na amewataka
wanachama hao kuendelea kuwa na umoja na ushirikiano ili kukamilisha ujenzi wa
ofisi kwa wakati.
Aidha mwenyekiti huyo ameonesha kufurahishwa na kitendo cha wanachama wa chadema jimbo la makambako kuanza ujenzi wa ofisi ya jimbo kwa kuchangishana fedha zao wenyewe bila kutegemea wafadhili na chama taifa na kueleza kuwa kitendo hicho ni cha uzalendo na itakuwa funzo kubwa kwa wanachama wengine nchini.
“Mmeipa changamoto wilaya nyingine nyingi zijifunze kutoka Makambako,na mnawajibu wale wanaosema Chadema hainaga ofisi,Chadema tuna ofisi mpaka za wilaya zaidi kama ya Makambako”alisema John Pambalu
Aliongeza kuwa “Tanzania hakuna Chama chocote cha siasa kuanzia CCM mpaka vyote vilivyobaki isipokuwa Chadema peke yake ambacho wanaweza wakajenga ofisi za Chama kwa nguvu ya wanachama bila hata ya Ruzuku”aliongeza Pambalu
Akizungumza kuhusiana na ujenzi wa ofisi hiyo
ambayo inajengwa mtaa wa makatani(kiumba) kata ya lyamkena ,Katibu wa chadema
jimbo la makambako ,DAUD TWEVE amesema kuwa wametenga kila siku ya
jumamosi kukukatana na kufanya maendeleo ya ujenzi wa ofisi hiyo na kueleza
kuwa lengo lao mpaka kufikia mwezi wa sita ofisi iwe imeezekwa.
“Lakini pia malengo yetu ni kwamba jingo letu hadi
kufikia mwezi wa sita tuwe tumelifunika,ofisi hizi tunajenga kwaajili ya kizazi
hiki na kinachokuja hata wanaccm wanafahamu majengo yao yale hawakujenga peke
yao na sisi tunaamini ofisi hii itatumika na watu wote”alisema Daud Tweve
Nao baadhi ya wanachama wa chama hicho cha CHADEMA
jimbo la makambako wamesema kuwa kukalika kwa ujenzi wa ofisi hizo kutaenda
kuboresha zaidi utendaji kazi wa chama hicho na kuepukana na gharama ambazo
zinatumika kwa sasa kulipa kodi ya pango kwenye ofisi ambazo wamepanga.
Zaidi ya milioni 50 zitatumika ili kukamilisha
ujenzi wa ofisi hiyo ambayo mpaka sasa ipo hatua ya renta.
0 Comments