TANGAZA NASI

header ads

Zao la thamani ‘Vanilla’ laanza kulimwa Njombe,wakulima wachangamkia



Na Amiri Kilagalila,Njombe


Wakulima kote nchini wamehamasishwa kuchangamkia fursa ya kilimo cha zao la vanilla ambalo uhitaji wake duniani ni mkubwa zaidi licha ya kwamba upatikanaji wa wa zao hilo kwa sasa umekuwa ni adimu.


Vanilla, Si zao ambalo limezoeleka haswa katika maeneo mengi nchini  licha ya kwamba si geni masikioni mwa wengi.    Ni zao ambalo uazalishaji wake umekuwa ni kidogo sana nchini pengine hata katika mataifa mengine kiasi kwamba gharama yake kwa sasa imepanda maradufu hadi kufikia shilingi mil.1 kwa kilo moja ya vanilla.


Kufuatia hali hiyo  Magreth Mgina meneja mahusiano wa kampuni ya Vanila International amechukua jukumu la kuhamasisha wakulima kuchangamkia fursa hiyo huku baadhi ya wakulima mkoani Njombe wakianza kuchangamka na fursa


“Tunawahamasisha sana wakulima hasa vijana kila mtu anayependa kujifunza na tunatoa elimu bure kuhusu kilimo hiki”


Zao la vanilla lina umuhimu haswa katika utengenezaji wa yoghati, keki vinywaji aina ya wine na vilevile maandazi.


Msanii uigizaji sauti maarufu ka jina la Baraka magufuli amepata nafasi ya kuzungumza na wakazi wa Njombe huku msisitizo akiuweka katika uzalishaji wa Vanilla.


“Niendelee kuhamasisha watanzania wote kwasababu mimi nimejionea hapa Njombe jinsi zao linavyplimwa,niombe tuhakikishe tunalima kwasababu zao hili pia lina thamani kubwa kwa sasa”alisema Baraka Magufuli


Uthubutu katika jitihada za kutafuta mafanikio ni hatua mojawapo katika kuyasogelea mafanikio, ambapo Gloria Haule huyu ni mama ambae amethubutu kujikita katika zao la vanilla, ameeleza matarajio yake katika kilimo hicho


“Kwa kweli mimi nilihamasishwa baada ya kusikia matangangazo hata kanisani,kwa hiyo matarajio yangu hapo baadaye niweze kufika mahali Fulani ambayo ni nzuri zaidi kuliko sasa”


Licha ya kuhamasisha wakulima kote nchini kuchangamkia fursa hiyo kampuni ya vanilla international inayopataikana katika maeneo ya kanisa la Anglican mjini Njombe,inatoa elimu bure kwa wale watao kuwa tayari kujikita katika zao hilo huku wakiwahakikishia upatikanaji wa soko kwa asilimia 99.9.


“Zao la Vanilla ni zao la fedha nyingi na kilo moja imeweza kufika mpaka zaidi ya milioni moja niwaombe sana wakulima kuwasiliana na sisi ili tuweze kuwasaidia katika kilimo”alisema Simon Mukondya mkurugenzi wa Vanilla International Ltd


Vanilla huchukua muda wa miezi mitatu tu tangu kupandwa hadi mavuno na gharama yake kila kilo moja inatajwa kufikia sh.laki 9 hadi mil.1 kwa sasa.


Post a Comment

0 Comments