TANGAZA NASI

header ads

Ujumbe wa Mo Dewji wamuamsha Kigwangalla "Tunataka Ushindi"

 


Baada ya kimya cha muda mfupi katika duru za soka nchini Tanzania kutokana na kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli.Hatimaye aliyekuwa waziri wa mali asili na utalii Dkt,Hamisi Kigwangalla ametoa ujumbe wa ushauri kwa Mwekazaji Muhamed Dewji juu ya uwekazaji wake ndani ya Club ya Simba.


"Bro, @SimbaSCTanzania tunataka ushindi, ndiyo raha yetu, hakuna kingine, na tunatambua mchango wako kwenye hilo. Tunakushukuru. Fuata makubaliano, tekeleza mkataba. Mimi ‘ulinishangaza’ kauli zako ndiyo maana nilihoji. We ni msomi/Mfanyabiashara, Unajua shida ilipo, rekebisha!"


Kigwangala ametoa ushauri huo katika ukurasa wake wa twita mara baada ya baadhi ya Jumbe kadhaa kutoka kwa mwekezaji huyo zikionekana kusambaa mitandaoni huku zikiwa zimeanza katika ukurasa wa twita wa mwekezaji Mo Dewji.


Baadhi jumbe mitandaoni zilizoandikwa na mwekezaji huyo ni pamoja na


"Tumetoka wapi tangu nimerudi @SimbaSCTanzania na tunaelekea wapi. Time will tell and history will be the judge. Narudia: issue ya Billioni 20 ntaongelea mchakoto wa transformation ukikamilika. If GOD gives me life, ntawashangaza critics."aliandika Mo Dewji


"Manchester United has agreed to a $305 million shirt sponsorship contract for 5 years. @SimbaSCTanzania doesn’t get even 1% of that with sports Pesa. Time has come to look out for better pastures." Aliandika tena Mo Dewji


Aidha kutokana na jumbe hizo baadhi ya wapenda soka nchini Tanzania na nje Tanzania wanaeleza kuwa mashaka na jumbe hizo huku wakidai huenda lipo tatizo katika uendeshaji wa Club hiyo.

Post a Comment

0 Comments