TANGAZA NASI

header ads

Ridhiwani aongoza msafara wa kuwafariji wahanga Pingo

 


Na Omary Mngindo, Pingo

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amewaongoza Mwenyekiti wa Halmashauri Geofrey Kamugisha na Mkurugenzi Mtendaji Ramadhani Possi, kwenda kuwafariji wakazi wa Kitongoji cha Pingo ambao nyumba zao zimebomolewa kwa upepo.

Msafara huo umetembelea eneo la Mbiki Kata ya Pera, ambao umeshuhudia nyumba 39 ambazo zimeangushwa huku nyingine zikihezuliwa paa kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali, iliyonyesha Machi Mosi mwaka huu.

Akizungumza baada ya kujionea athari hiyo iliyohusisha na mikorosho iliyoangushwa kufuatia mvua iliyoambatana na upepo, Ridhiwani alisema kuwa wamepewa taarifa na uongozi wa Serikali kuhusiana na athari hiyo.

"Tulijulishwa na uongozi wenu

kutokea kwa tukio hili, tumekuja tumejione hali halisi poleni sana kwa kadhia hii, tumeona yapo mambo yaliyo ndani ya uwezo wa halmashauri tutayafanyiakazi, yaliyo juu yetu tutayawasilisha Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kuona ni namna gani tunasaidiana" alisema Ridhiwani.

Kamugisha alisema kuwa wamefika kwa lengo la kuwapa pole kwa tukio hilo, huku akieleza kwamba wamejionea nyumba 39 zilizokumbwa na maafa hayo, ambapo amewapa pole na kueleza kuwa wanakwenda kukaa kuona ni namna gani wanaweza kuungana nao katika hilo.

"Tukiongozwa na Mbunge Ridhiwani,  Mimi na Mkurugenzi Possi na wataalamu wetu tutakwenda kukaa kuona ni namna gani tunavyoweza kushirikiana katika kusaidiana kwenye janga hili, tunawapa pole endeleeni kuwa watulivu Serikali yenu tupo pamoja nanyi," alisema Kamugisha. 

Nae Possi alisema licha ya kuona hali halisi, yupo tayari kupokea maelekezo ya viongozi hao kisha kufanyia kazi aliyoyaona katika tukio hilo ili kuona ni naamna gani watakavyochukua hatua za haraka.

"Poleni sana kwa kadhia hii, tunaungana nanyi katika kuwapa pole kwa matatizo ambayo mmeyapata tunawahakikishia tupo pamoja nanyi katika tunakwenda kukaa ili kuona ni namna gani tutasaidiana," alisema Possi. 

Wahanga Mariam Salehe na Muhidini Rashid walimpongeza Mbunge na msafara wake kwa kufika eneo hilo kuwafariji, huku wakiwaombea baraka katika uongozi wao ili waendelee kuwatumikia wana-Chalinze wote.

"Tunawaombea dua muendelea kuwatumikia wananchi usiku na mchana, kitendo chako Mbunge Ridhiwani kuambatana na viongozi wenzako kuja kutufariji kimetuongezea imani kwenu, tunawashukuru sana," alisema Mariamu.

Post a Comment

0 Comments