TANGAZA NASI

header ads

Misri 'yaagiza kukamatwa' kwa madereva wa treni baada ya ajali



 Mamlaka nchini Misri imeamuru kukamatwa kwa watu wanane kufuatia ajali ya treni ya wiki iliyopita iliyosababisha vifo vya watu 18, Shirika la habari la AFP limeripoti, likinukuu ofisi ya mwendesha mashtaka.

"Mwendesha mashtaka mkuu ameagiza madereva wawili... wasaidizi wao wawili, mlinzi wa mnara wa kudhibiti trafiki, mkuu wa kudhibiti trafiki katika mji wa Assiut na walinzi wengine wawili... kuzuiliwa," AFP limemnukuu mwendesha mashtaka.

Mabogi ya treni hiyo yaliondoka katika reli na kuanguka bada ya treni mbili kugongana katika mji Tahta mkoani Sohag siku ya Ijumaa.

Idadi ya vifo katika ajali hiyo imepunguzwa hadi watu 18 alisema Waziri wa Afya Hala Zayed, kutoka watu 19.

Awali ilikuwa imeripotiwa ni watu 32 waliopoteza maishaisha pindi baada ya ajali hiyo kutokea.

Misri imeshuhudia ajali za treni za mara kwa mara kutokana na mifumo duni ya reli na ukosefu wa uwekezaji katika usafiri wa treni.

Post a Comment

0 Comments