NA HADIJA OMARY
Meneja wa Shule ya Muungano Day Care Mariamu kadangu amesema kuwa kupitia Ugonjwa wa Corona Shule yao imepata mbinu mpya ya Ufundishaji hasa watoto wanapokuwa katika kipindi cha Likizo inayowawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza wakiwa nyumbani
Kadanga ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa anazungumza na Njombe press blog ilipotembelea Shuleni hapo na kutaka kujua ni kwa namna gani waliweza kuwaelekeza wanafunzi hao watakapokuwa majumbani kwao masomo yote ambayo walikuwa wanafundishwa na walimu darasani watayasoma kwa njia ya mtandao.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2020 wakati ugonjwa wa Covid 19 ulipo ingia Nchi nyingi zilikubwa na taharuki kiasi kwamba baadhi ya Nchi hizo Wananchi wake waliwekwa karantini ambapo kwa Nchini Tanzania pamoja na jitihada za kujikinga na kujilinda na ugonjwa huo serikali iliamulu kufunga shule kwa Muda usiojulikana mpaka pale Ugonjwa huo utakapo isha
Katika kipindi hicho Walimu walijitahidi kubuni mbinu mbali mbali za ufundishaji kwa wanafunzi wao wakiwa bado wapo Nyumbani ili hata shule zitakapofunguliwa wanafunzi wasiwe nyuma katika masomo.
Shule hiyo ya Muungano day Care ni miongoni mwa Shule zilizokuwa zimebuni mbinu mbadala ya ujifunzaji wa wanafunzi wao katika kipindi cha likizo hiyo ya Corona
Kadangu alisema pamoja na vifurushi walivyovitoa kwa Wanafunzi hao lakini pia kwa kuwapa vitabu vyenye picha mbali mbali viliwafanya watoto wadogo wanaosoma Madarasa ya Awali kuwasaidia kujikumbusha mambo mbali mbali Wanayojifunza wakiwa shuleni.
" Njia hii kwetu ilikuwa mpya ambayo hatukuwa tukiitumia huko nyuma lakini tumegundua kutumia kwa mbinu hii kunawawezesha watoto kutosahau vitu hata watakaporudi likizo pindi shule zinapofungwa na kusalia nyumbani" alisema Kadangu
Kadangu pia alisema kuwa Mbinu hiyo ya Ufundishaji itaendelea kutumika hata kipindi cha likizo za kawaida kwani wamegundua imekuwa msaada mkubwa kwa Wanafunzi wao.
Mariamu Saidi ni mmoja wa wazazi ambae Mtoto wake anasoma katika Shule hiyo ya Muungano ambapo ameeleza kuwa kutokana na vifurushi hivyo walivyopewa watoto hao haikuwa kazi ngumu kwao kusaidia watoto kujifunza .
0 Comments