TANGAZA NASI

header ads

MEYA SONGEA AWAONYA WAZAZI WANAOTELEKEZA WATOTO KIPINDI CHA MASIKA

 


Joyce Joliga,Songea


Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano amewaonya  baadhi ya Wazazi na walezi wanaotelekeza Watoto wadogo na kuwaacha pekee yao wajilee kipindi hiki Cha Masika kwa kuhamia mashambani kuwa wataanza kuchukuliwa hatua.

Akizungumza na Mwandishi wa Blog hii Mbano amewataka Wenyeviti  wa mitaa  kuanza kuwachukulia hatua wazazi ambao wanaotelekeza Watoto kwenye mitaa yao.

Amesema, Wazazi wawajibike na kuwalea Watoto wadogo bila kuwaacha wajilee wenyewe kwani jukumu la Ulinzi na usalama wa mtoto ni lao.

" Nitapita kufanya mkutano na wazazi pamoja na Walezi Katika kata mbalimbali  ili niongee nao na kuwaelimisha umuhimu wa kuwalinda Watoto kwani wanapowatelekeza na kuwaacha pekee yao wanaweza kupata matatizo mbalimbali,"Alisema

Amesema, Watoto wanapoachwa peke yao ni hatari kwani wanaweza kuugua au kuvamiwa na wakashindwa kujitetea,ikiwa ni pamoja na kushindwa kuhudhulia Masomo yao.

Kwa upande wake Mwanahamisi Mkotya Mkazi wa Ruhuwiko amesema ipo haja ya wazazi kuanza kushitakiwa kwa tatizo la Wazazi kutekeleza Watoto limekuwa likiongezeka siku hadisiku na kuwataka wazazi kuacha vitendo hivyo

Naye Diwani kata ya Ruhuwiko Wilbert Mahundi amesema jamii iwafichue wazazi hao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwani kutelekeza watoto ni kosa kisheria ambapo amewataka wazazi kuwapenda na kuwalea watoto wao  na kuacha kuwanyanyasa kwa kisingizio cha kilimo.


Aidha ameishauri jamii kuanza kuwabana wazazi wenye tabia hizo waliopo kwenye maeneo yao.

Naye Jonathan Mhenga Mkazi wa Namtumbo ameiomba Serikali kutunga Sheria ndogo za kuwabana wazazi ambao hawawajibiki kwa Watoto wao.


Post a Comment

0 Comments