TANGAZA NASI

header ads

Watoto wenye ulemavu wa macho na ngozi waomba msaada kwa jamii ili kutimiza ndoto zao

 


Joyce Joliga,Songea


 Wanafunzi wenye ulemavu wa macho  na ngozi wa shule ya msingi Ruhila Mchanganyiko Manispaa ya Songea  wameiomba jamii kuwa mstari wa mbele ,katika kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili,kwa madai kuwa changamoto hizo zisipopata ufumbuzi,zinarudisha nyuma ufanisi wao katika kuisaka elimu.


Ombi hilo limetolewa Kwa mmoja wa wanahabari mkoani Ruvuma,wakati alipotembelea shuleni hapo ,kwa lengo la kutoa msaada wa vyakula,kwa wanafunzi hao wenye mahitaji maalum 35 wa shule hiyo..


Akizungumza na Mwandishi wa Blog hii Mwanafuzi Dorcas Gwasi  amewaomba watu kuwasaidia na si kuiachia serikali pekee kwani shule hiyo inawatoto wadogo ambao wanahitaji kupata malezi na kusaidiwa kama watoto wengine.


Alisema, watoto wanahitaji sukari, mafuta ya kupaka ya kawaida nay a wenye ulemavu wa ngozi (Albino)pia sare za shule.


Nikson Omangi ni  mkuu wa kitengo cha ulemavu shule ya msingi Ruhila anasema richa ya Wanafunzi hao kuwa jukumu la kuwasaidia watoto hao si la mtu mmoja bali la jamii nzima.


Alisema, watoto hao wanahitaji faraja toka kwa jamii ,na kuwataka watu wenye mema kuwatembelea na kuwafariji kwa kuwapatia vitu vidogo vidogo ikiwemo madaftari, chakula na hata nguo kwani wapo ambao hawana huwezo .


“Tuna huyu mtoto wa kike wa  miaka 5 ameletwa hapa shuleni  juzi ni yatima hana nguo wala sare za shule ,mnavyomuona ndivyo alivyo hivyo mtaona namna watoto hawa wanavyohitaji msaada wa jamii ,tusiwape kisogo bali tuwasaidie kwani nao wanahitaji kutimiza ndoto zao,”alisema


Gosberth Nduguru ni  Mwalimu mkuu wa shule hiyo anasema  bajeti inayoletwa na serikali haikidhi mahitaji yote ya watoto hao hivyo wanaomba watu wenye uwezo wawasaidie watoto hao.


 


Post a Comment

0 Comments