TANGAZA NASI

header ads

RASMI NDAYIRAGIJE AFUTWA KAZI STARS

 


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF), limetangaza rasmi kuachana na kocha wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije kwa makubaliano ya pande zote mbili.

Akizungumzia uamuzi huo, Ofisa habari wa TFF Clifford Marion Ndimbo amesema wanamshukuru kocha huyo, na tayari mchakato wa kumsaka mbadala wake umeanza ambapo atatangazwa muda wowote kuanzia sasa.

“Baada ya kikao cha pamoja na kocha Etienne Ndayiragije, pande zote mbili zimefikia makubaliano rasmi ya kuvunja mkataba.

“Tunamshukuru kocha Ndayiragije kwa kazi yake kipindi chote alichoifundisha Stars, mchakato wa kumtangaza mbadala wake unaendelea na atatangazwa muda wowote kuanzia sasa,”

Hii hapa taarifa ya TFF;

Post a Comment

0 Comments