TANGAZA NASI

header ads

Elimu ya VVU yazidi kukolea kwa wanafunzi Makambako

 


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Ili kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU) mjini Makambako mkoani Njombe,wanafunzi wa kike kutoka shule ya sekondari Makambako wamefanikiwa kufikiwa na kupata mafunzo dhidi ya virusi vya ukimwi ili waweze kuhamasika katika upimaji wa hiari na kutambua afya zao.


Hamis Kasapa ni mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali Umbrela of Women and Disabled Organization (UWODO),amesema katika mradi wao wa mwaka mmoja chini ya ufadhili wa mfuko wa Rais ubalozi wa Marekani (PEPFA),wanaendelea kuhamasisha wasichana pamoja na kuwajengea uwezo ili kuendelea kujikinga na virusi vya ukimwi.

“Tunaamini hawa mabinti tukiweza kuwapa elimu,wataweza kuwa na ujasiri wa kuweza kuongea na wanaume na kuwaambia bado wanasoma na hawajafika kwenye ndoto zao,kwahiyo leo tuko Makambako kwa ajili ya kuhamasisha waweze kwenda kupima,waweze kupata milo kamili ili kama kuna mtu anaishi na maambukizi aweze kukimbizana na ndoto zake”alisema Hamis Kasapa

Fausta Minzi ni mtaalamu wa afya aliyeongozana na ujumbe kutoka shirika hilo,ameendelea kutoa rai kwa wadau na serikali kuendelea kushirikiana ili kuwafikia vijana kutoa elimu ili kupunguza hatari zaidi ya maambukizi.

“Tusipoweza kuwafikia hawa vijana na kutoa elimu ya jinsi gani ya kuepukana na HIV  na kujiepusha na mapenzi katika umri mdogo itakuwa ni hatari sana na ni rahisi kwo kupata maambukizi kwasababu watakuwa hawajui ni kitu gani wafanya ili kuepukana na vishawishi”alisema Fausta Minzi

Naye Godluck Kinyunyu ni makamu mkuu wa shule ya sekondari Makambako,anasema wataendelea kualika wadau ili kutoa elimu ya kujitambua kwa wanafunzi.

“Tumekuwa tukikaa nao mara nyingi na tukialika wadau mabali mbali wanaoweza kutoa elimu ya jinsia ili kuhakikisha wanapata elimu ya kujitambua ili kuongea nao na kuona ni namna gani wanajitambua na kuepukana na vishawishi vinavyowafanya wasitimize malengo yao”alisema Mwl.Godluck Kinyunyu

Editha Mdegela na Tupokela Liko ni miongoni mwa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo,wanasema wamefurahishwa na kuipokea elimu inayohusu maambukizi kwa kuwa kumekuwa na vishawishi vikubwa kutoka kwa wanaume na kujiingiza kwenye mahusiano bila kujali kanuni za afya.

“Tunashukuru kwa elimu kwa kuwa tunakabiliana na vishawishi vingi utakuta huko barabarani tunasimamishwa na kushawishiwa hata kwa pesa na kudanganyika halafu mwisho wa siku tunaingia kwenye matatizo”aliseama Editha Mdegela

Post a Comment

0 Comments