TANGAZA NASI

header ads

China yaanza kuwafundisha vijana ukakamavu

 


Tangazo kutoka wizara ya elimu nchini China limesababisha gumzo baada ya kusema kuwa vijana wadogo nchini China wameanza kuwa na tabia za "kike".

Taarifa hiyo imekosolewa kama yenye ubaguzi wa kijinsia na watumiaji wa mitandao - lakini baadhi wanasema kuwa kwa kiasi fulani wasanii wa kiume wanastahili kulaumiwa.

Kwa kipindi fulani, serikali ya China imeonesha wasiwasi wake kwamba wanaume maarufu kama vile wanariadha, wanajeshi mashujaa na wengine ambao wangekuwa mfano mwema wa kuigwa hawapo tena.

Hata Rais Xi Jinping ambaye anafahamika kama shabiki wa mpira, kwa kipindi kirefu amekuwa akitoa wito wa kukuza vipaji watakao kuwa mfano wa kuigwa katika michezo.

Wiki iliyopita, wizara ya elimu ilitoa tangazo lililokuwa na kichwa chenye kuelezea kinaga ubaga lengo lake.

Pendekezo la kuzuia vijana waliobalehe kuwa na tabia za kike lilitoa wito kwa shule kubadilisha kabisa wanachofunza katika masomo yao na kuimarisha usajili wa walimu.

Ujumbe huo ulishauri usajili wa wanamichezo waliostaafu na watu wenye historia ya michezo - na kuendeleza michezo mingine kama vile kandanda kwa lengo la "kukuza sifa za kiume".

Ni hatua iliyoazimiwa katika nchi ambayo vyombo vya habari haviruhusu kingine chochote zaidi ya kile ambacho ni kisafi kabisa, "nyota" wanaowajibka katika jamii.

Lakini kulikuwa na dalili za awali zilizoashiria kuwa hatua hiyo inakaribia. Mwezi Mei mwaka jana, mjumbe kutoka bodi ya juu ya ushauri, Si Zefu, ilisema kuwa vijana wengi wa China wamekuwa, "dhaifu, wenye uoga na kujidhalilisha".

Kulikuwa na mtindo miongoni mwa vijana wa China wa kuwa na tabia za "kike", Si Zefu alidai, ambako bila shaka "kutahatarisha uwepo na maendeleo ya taifa la China" tatizo hilo "lisipodhibitiwa kikamilifu", aliongeza.

Si Zefu alisema kuwa mazingira ya nyumbani kwa kiasi fulani yanastahili kulaumiwa kwa hilo, huku wavulana wengi wa kiume wakilelewa na mama zao au bibi zao.

Pia alisema kuwa ushawishi wa baadhi ya wasanii wa kiume uneondelea kuongezeka, kumefanya watoto wengi kutotaka tena kuwa mashujaa katika jeshi tena.

Kwahiyo, akapendekeza kwamba shule zinastahili kuchukua jukumu kubwa kuhakikisha vijana wa China wanapata elimu yenye uwiano

Post a Comment

0 Comments