TANGAZA NASI

header ads

Matukio ya ukatili wa watoto yapungua Makambako



Na Mwandishi wetu, Njombe

Jamii imetakiwa kuendelea kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya dola  ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

Hayo yamesemwa na afisa ustawi wa jamii halmashauri ya mji wa Makambako MASINDE MASINDE wakati akizungumza na kituo hiki ofisini kwake  ambapo amesema licha ya matukio hayo kupungua kwa sasa lakini jamii ina kila sababu ya kuendelea kuyakemea na kushirikiana na serikali ili kuwafichua wanaotekeleza matukio hayo.

Aidha Masinde amesema jamii inatakiwa kutambua kuwa watoto wadogo wanapaswa kulindwa hivyo inalojukumu la kuwalinda,kuwapenda na kuwathamini ili waweze kuja kutimiza ndoto zao.

Hata hivyo amesema watoto walio na umri chini ya miaka kumi na mbili wamekuwa wahanga wakubwa wa matukio ya ukatili kwa kuwa umri huo wanashindwa kujitetea.

Nao baadhi ya wakazi wa halmashauri ya mji wa Makambako wamekiri kuwa jamii inajukumu kubwa la walinda watoto ili kuja kuwa na jamii bora siku za baadae huku wakiitaka serikali hususani maafisa ustawi wa jamii kutoa elimu zaidi ya namna ya kushiriki kutoa taarifa za matukio ya ukatili wanaofanyiwa watoto.

 

Post a Comment

0 Comments