TANGAZA NASI

header ads

Ziara ya kushtukiza ya Jokate yajibu watu 327

 


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, amesema baada ya ziara yake kwenye ofisi za TANESCO Kisarawe tarehe 13.01.2021, kati ya wananchi 332 waliofika siku hiyo kuomba 'control number' wananchi 327 walipatiwa siku hiyo hiyo na waliobaki walipatiwa siku inayofuata.

Pia wananchi 380 waliandikishwa Mita zao kwa ajili ya kufanya malipo ya huduma ya umeme.

Aidha Jokate ameongeza kuwa maombi ya nyuma 974 ya 'control number' yanafanyiwa kazi ngazi ya wilaya kwa kushirikiana na mkoa kuhakikisha mpaka Jumatatu wananchi wote watapatiwa.

Pia ameeleza kuwa wananchi 380 waliandikishwa mita zao kwa ajili ya malipo ya huduma ya umeme.

Amemaliza kwa kusema, ''Hii ni taarifa ya awali tunaendelea kushughulikia kero zenu zote. Inawezekana. Poleni sana wananchi wanaohudumiwa na Kisarawe kwa changamoto hii, Kama watumishi wenu tutaendelea kuhakikisha tunafuatilia changamoto mbalimbali kwenye taasisi zetu za umma na hata binafsi. Hapa Kazi Tu''

Post a Comment

0 Comments